ALICHOKISEMA DIAMOND KUHUSU MPENZI WAKE MPYA.
Mwimbaji Diamond Platnums amekiri kwamba kwa sasa ana mpenzi mpya ambae sio maarufu kabisa.
Ameamplfy
kwamba “tuna kama mwezi hivi toka tumeanza kuwa pamoja, sio vizuri sana
kumzungumzia kwa sababu naogopa sana drama mwisho yasije yakawa yale
yale tena ndio maana nafanya siri lakini sio maarufu na wala sio Jokate”
millardayo.com
ilipomuuliza kama ataingia tena kwenye mapenzi na mtu maarufu ambako
ndiko alikotoka, Diamond amesema “kwa kweli siwezi kujua kwa sababu kila
kitu kinaandikwa na mapenzi ni kama ajali”
Diamond
aliwahi kukanusha exclusive on millardayo.com kwamba hana uhusiano wa
kimapenzi na mrembo Jokate ambae walianza kuzungumziwa sana baada ya
Jokate kushuka kwenye gari moja na Diamond wakati wakiwasili kwenye show
ya Mlimani City wiki kadhaa zilizopita.
Kwenye
hiyo benz alishuka Diamond na mama yake mzazi pamoja na Jokate na
Diamond alipoulizwa na millardayo.com alisema siku hiyo alitakiwa
kushuka na mamodo wawili lakini mmoja ambae ni Lisa alishindwa kuja siku
hiyo kwa hiyo ikabidi ashuke na Jokate tu.
Kwa hisani ya millardayo
إرسال تعليق