THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
|
Telephone: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: ikulumawasiliano@yahoo.com
Fax: 255-22-2113425 | ![]() |
PRESIDENT’S OFFICE,
THE STATE HOUSE,
P.O. BOX 9120,
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
|
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
RAMBIRAMBI
Rais Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia salamu za rambirambi Mwenyekiti wa klabu ya mpira wa miguu ya Young Africans Sports Club (Yanga) Bw.
Lyod Nchunga kufuatia kifo cha Mjumbe wake wa Kamati ya Utendaji,
wakili Theonist Rutashoborwa, aliyefariki dunia usiku wa kuamkia leo
kutokana na ugonjwa wa Shinikizo la Damu na Kisukari.
“Nimepokea
kwa Masikitiko na huzuni sana taarifa za wakili Theonist Rutashoborwa
kilichotokea usiku wa Kuamkia leo, hili ni pigo na pengo kubwa katika
klabu ya Yanga katika kipindi hiki cha kushiriki ligi kuu” Rais amesema.
“Naomba
unifikishie rambirambi zangu za dhati kwa familia, wachezaji na wana
Yanga wote kwa kuondokewa na Mjumbe wao katika kipindi hiki”
Rais ameongeza na kuwataka wana Yanga wawe wavumilivu wakati wa msiba
huu na kumuombea Bw. Rutashoborwa mapumziko mema ya Milele.
……………Mwisho…………
Imetolewa na Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais, Msaidizi.
Ikulu-Dar-Es-Salaam
12 April, 2012

إرسال تعليق