Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Arusha ahamia Chadema
Aidha
alisema hawezi kuendelea kupanda gari lenye pancha lukuki,
hivyo ameamua kupanda gari lisilo na pancha na lenye kutoa matumaini
mapya kwa watanzania.
Hayo ameyasema leo, wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye Hoteli ya Kibo Palace, iliyopo Jijini hapa.
Amesema
mara nyingi alikuwa akikemea mambo ambayo yanaweza kubomoa chama cha
CCM kwa upendo, lakini alikuwa akipuuzwa kwa sababu ya chama hicho kuwa
na kikundi cha wenyewe.
“Mimi
nanukuu maneneo ya Nyerere kuwa alishawahi kusema CCM sio mama yangu na
mimi pia CCM sio mama yangu na natangaza rasmi, kuondoka ndani ya chama
hiki na najiunga na Chadema, sababu ndicho chama chenye kuleta tumaini
jipya kwa watanzania,”alisema.
Ametaja
nafasi alizoachia ngazi ni pamoja na Mjumbe kamati ya utekelezaji UVCCM
Taifa, Mjumbe kamati ya siasa Mkoa na Mjumbe Halmashauri Kuu CCM Mkoa.
Amesema
kuwa inasikitisha kuona Vijana wa UVCCM Mkoa wa Pwani, wanatoa matamko
kuwa Rais ajaye 2015 hatatoka kanda ya Kaskazini na anayemfahamu ni Rais
peke yake ambaye ni Jakaya Kikwete.
Millya
alisema cha kusikitisha pale alipokemea kauli hiyo alipuuzwa na hadi
sasa Ikulu haijawahi kutoa kemeo kwa Vijana hao na wala kukataza kauli
hizo kutolewa, jambo lililompa jibu kuwa Ikulu inahusika kwa namna moja
au nyingine na kauli hiyo.
Aidha
alisema kuna Vijana wengi walioko ndani ya CCM wakiishi kwa matumaini
ya kusubiri kuteuliwa nafasi ya Mkuu wa Wilaya kama sio Mkoa, ila yeye
hawezi kuishi kw amatumaini kama muathirika wa Ukimwi.
Hata
hivyo alitoa wito kwa Vijana wote wenye nia ya dhati na mapenzi mema ya
nchi yao, kumfuata Chadema ambako kunatoa tumaini jipya la maisha ya
watu.
Millya
ambaye alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa UVCCM tangu 2008 hadi sasa,
aliwashukuru vijana kwa kumpa ridhaa hiyo na ataendelea kuwashukuru,
ila ameamua kwa ridhaa yake kuachia ngazi zote kwa ajili
ya ukombozi wa kweli.
Millya
hivi karibuni alijitosa kinyang’anyiro cha kugombea Ubunge wa Afrika
Mashari ndani ya Chama chake cha CCM, lakini alichijiwa baharini na
kutolewa jina lake.
Wakati
Kiongozi huyo akitangaza kuachia ngazi hiyo ya juu ya UVCCM,ndani ya
Chama cha CCM, Mkoa wa Arusha, Vijana mbalimbali wameonekana kutoamini
walichosikia na wengi wao wakionyesha nia ya kumfuata.
Akizungumza
kwa niaba ya vijana wenzake, Hamisi Bakari, alisema kuwa amesikitishwa
na kiongozi wake kuhama chama na hiyo inaonyesha CCM imeoza na hivyo
kilichobaki hata wao kumfuata anakokwenda.
“Mimi
na wenzangu tutakwenda huko aliko kwa sababu kama yeye kiongozi ameamua
kujiunga Chadema hata sisi wadogo hatuna mana ya kuendelea kubaki
huku,”alisema.
Habari na Rosemary Kitosia, Arusha yetu.blog
إرسال تعليق