Kikosi Cha Zimamoto Zanzibar Chazindua Kifaa Kipya DSPA 5
Kamishna Ali Abadalla Malimussa kushoto akiangalia kifaa kipya cha
kuzimia moto kijulikanacho kama DSPA 5 kutoka kwa askari wa kikosi cha
Zima moto na uokozi katika hafla ya uzinduzi wa kifaa hicho Maisara
mjini Zanzibar
Frans Volgelzangs ambaye ni mtaalamu wa Kampuni ya AFG inayozalisha
kifaa kipya cha kuzimia moto ania ya DSPA5 akitoa maelezo jinsi ya
kukitumia kifaa hicho.
Mkurugenzi wa mtendaji wa Kampuni ya Your Solution Tanzania LTD Damian
George kushoto akimkabidhi kivaa kipya DSPA 5 Naibu Waziri wa Miundo
mbinu na Mawasiliano Zanzibar Issa Haji Gavu katika hafla ya uzinduzi wa
kifaa hicho Maisara mjini Zanzibar.
Picha zote na Iddi Haji-Maelezo Zanzibar na Ali Issa-Maelezo
---
IMETOLEWA NA
Kikosi cha Zima moto na uokozi Zanzibar (KZU) kimezindua kifaa kipya
cha kisasa chakuzimia moto kiitwacho Dry Sprinkler Powder Aerosol (DSPA
5),ambacho huzima moto ndani ya dakika mbili baada ya kifaa hicho
kukitumbua fyuzi zake kwa sekunde nane.
Uzinduzi huo umefanyika Maisara Mjini Zanzibar mbele ya Naibu Waziri wa
Mawasiliano na Uchukuzi Issa Haji Gavu pamoja na makamanda mbalimbali
wavikosi vya SMZ na makamishina kutoka vikosi vyote.
Katika uzinduzi huo Kamishina wa kikosi hicho Ali Abdalla Malimusa
alisema kuwa kifaa hicho kimekuja wakati muafaka kwavile kumekuwa na
matukio mbali mbali ya kuwaka kwa majengo ya Serikali, nyumba za watu
binafsi na Ofisi za kiraia ,hivyo kifaa hicho kitakuwa muokozi wa maafa
hayo iwapo yatatokea.
Amesema Zanzibar ni Taifa linalohitaji mabadiliko ya kidunia ili kwenda
sambamba na dhana za kisasa za uokozi pale ambapo pametokea janga la
moto na kwamba hakuna budi kupambana nalo bila ya kuleta maafa .
“Nikifaa muhimu kwani hakitumii maji kitasaidia kwa kiasi kikubwa
nchini kwetu kwani sisi ni sehemu ya dunia ”alisema Kameshina Ali
Abdalla .
Nae Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya ‘Your Solution Tanzania LTD’
ambayo imeshirikiana na AFG Group ya Uholanzi Damian Geoge akitoa
ufafanuzi wakifaa hicho cha DSPA alisema kuwa lengo hasa la kifaa hicho
ni kuwaonesha Wazanzibari na Watanzania kwa ujumla namna ya kukitumia
pale litatokea janga la moto.
Alisema DSPA ni tekinolojia ya kisasa ambayo haina madhara yoyote ya
kiafya wakati wa uzimaji moto hata pale mtu atakapokuwa yupo ndani
wakati wa kuzima moto .
Amesema kifaa hicho kwa nchi za Afrika, Tanzania imekuwa nchi ya kwaza
kufika ambacho huzima moto kwenye chumba chenye ukubwa wamita 100 za
mraba kwa Dspa 5 moja yenye uzito wakilo moja .
Kifaa hicho kina uwezo wa kudumu kwa miaka 15 bila ya kuharibika baada
ya kukinunua.
IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR
إرسال تعليق