Angalia Maandalizi ya Killi Music Award 2012
Kinyang’anyiro
hicho ambacho kilianza takriban miezi mitatu iliyopita kilizinduliwa
kwa sherehe kali, baada ya hapo kamati ya tuzo ilichagua wana akademi
wapatao 50 ambao waliingia kambini siku 2 kwa ajili ya kufanya mchujo wa
wasanii ambao walitakiwa kuingia katika kinyang’anyiro hicho.
Msanii Nasib Abdul almaarufu kama Diamond Platnumz anaongoza
kinyang’anyiro hicho akiwa anawania tuzo 7 akifuatiwa na msanii Ali Kiba
ambaye anamfuatia kwa karibu huku akiwania tuzo 5.
Swali lilopo kwenye vichwa vya watu ni je msanii Diamond ataweza vunja
rekodi iliyowekwa na msanii 20% aliposhinda tuzo 5 mwaka jana na pia
msanii huyo ataweza kumbwaga msanii mwenzake Ali Kiba??
Picha kwa hisani ya Bongo 5


إرسال تعليق