Mafunzo ya waandishi wa habari TGNP

WAANDISHI wa habari wameaswa kubeba sauti za
wananchi walioko pembezoni katika kudai haki zao hasa wakati wa
mchakato wa kukusanya maoni ya wananchi kwaajili ya kuandaa katiba mpya.
Akizungumza
Kaimu Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Jinsia kilichoko chini ya Mtandao wa
Jinsia Tanzania (TGNP) Dorothy Mbilinyi, amesema watanzanzia masikini
walioko pembezoni wanategemea kupata taarifa na kutoa taarifa kupitia
vyombo mbalimbali vya habari.
“
Wananchi wameamka wameanza kujieleza vyombo vya habari vinatakiwa
kufanya kazi yake kuwa sauti ya wanyonge, viwe mdomo kwa makundi
yaliyowekwa pembezoni, ili kuibua changamoto zilizojificha na kuyafanya
makundi haya kuwa na haki sawa na wengine,” amesema Mbilinyi
Mbilinyi amesema kuwa vyombo vya habari vya Tanzania vimefanya kazi
kubwa ya kuibua kero za wananchi na ufisadi, ikiwepo kudai uwajibikaji
katika misingi ya demokrasia na haki za biandamu.
Aidha
amewataka waandishi wa habari kufanya kazi kwa bidii mwaka huu
kwasababu ni mwaka wenye changamoto nyingi ambazo zitahitaji weledi,
uadilifu, ukweli na uwazi.” Huu nini mwaka wa kukusanya maoni ya katiba,
mwaka wa kudai uwajibikaji kwa viongozi wasio waadilifu, na ni mwaka wa
Sensa ya idadi ya watu…” amesema Mbilinyi.
Akieleza malengo ya mafunzo hayo ya siku tatu yaliyoanza mei 3 hadi 5,
Mkuu wa Idara ya Mawasiliano na habari, Lilian Liundi amesema kuwa
mafunzo hayo yatawasaidia waandishi wa habari kujitadhimini upya jinsi
ambavyo wanaandika habari za kijinsia.
Pamoja
na kujitadhimini waandishi wa habari watajifunza juu ya hali ya sasa
ya ujenzi wa vuguvugu la ukombozi wa wanawake kimapinduzi, kampeni ya
haki uchumi, mfumo dume na mfumo uleberali mambo leo.
Pia watajifunza namna ya kuandika habari za kijinsia na kuchambua maoni
yanayotolewa na wananchi juu ya katiba mpya, kufanya habari za
kiuchunguzi vijijini na kuibua changamoto za wananchi.
Mafunzo
haya yanafanyika ikiwa ni siku chache baada ya TGNP kukutana na
wahariri wa vyombo vya habari jijini Dar es alaam wiki iliyopita.
إرسال تعليق