
Watu wakiomboleza shambulio katika soko moja nchini Nigeria
Watu 34 wameripotiwa kuuawa na
wengine 29 kujeruhiwa kufuatia shambulio katika mnada wa ng'ombe mjni
Postiskum, Kaskazini mwa Nigeria.
Utawala wa nchi hiyo umesema kuwa shambulio hilo
lilikuwa ni la kulipiza kisasi kwa mauaji ya mtu mmoja yaliyofanywa na
wafanyabiashara waliomtuhumu kutaka kuiba ngombe katika soko hilo.
Mifugo
wengi wanasemekana kuteketea hadi kufa. Potiskum ni moja ya mji
Kaskazini mwa Nigeria ambayo yamekumbwa na mashambulio ya mara kwa mara
yanayotekelezwa na wapiganaji wa Kiislamu wa Boko Haram.
Mtu mmoja ambaye alikuwa katika soko hilo wakati
wa uvamizi huo, ameiambia BBC kuwa watu waliokuwa wamejihami kwa
bunduki, washambulia soko hilo jana usiku wakitumia mabomu huku
wakiteketeza vibanda vilivyojengwa.
Milio ya milipuko na moto huo ulisababisha hali
ya wasi wasi miongoni mwa wachuuzi katika soko hilo, ambao walianza
kutoroka kutoka eneo hilo.
Wavamizi hao waliziba milango yote ya soko hilo na kuwafyatulia risasi wale waliokuwa wakitoroka.
Msemaji wa kikosi maalum ya jeshi ambalo limetumwa katika eneo hilo, amesema wanashuku wapiganaji wa Kiislamu wa Boko Haram.
Kanali Dahiru Abdussalam, amethibitisha kuuawa
kwa watu 34, lakini baadhi ya wafanya biashara wanasema huenda idadi
hiyo ikaongezeka na kufikia watu 50.
Serikali ya nchi hiyo imekanusha madai kuwa,
jeshi lilifahamishwa kuhusu tishio la kutokea kwa shambulio hilo na
halikufanya lolote kuzuia ili kuokoa maisha.
Chanzo:- BBC Swahili
إرسال تعليق