Pichani
Juu na Chini ni Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Balozi Khamis
Kagasheki (kulia) akizungumza wakati akitoa tamko la kuwasimamisha kazi
baadhi ya watumishi wa TANAPA ili kupisha uchunguzi dhidi ya mauaji ya
Faru wawili. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Wanyamapori Pauli Sarakikya.
Waziri
wa Maliasili na Utalii Mh. Balozi Khamis Kagasheki amewasimamisha kazi
vigogo wanne na watumishi kadhaa ili kupisha uchunguzi ufanyike kufuatia
tukio la wanyapori wawili aina ya Faru kuuawa katika Hifadhi ya Taifa
ya Serengeti eneo la Moru.
Mh.
Balozi Kagasheki amewataja vigogo hao kuwa Kaimu Mkurugenzi wa Uhifadhi
wa TANAPA Justin Mhando, Mkuu wa Kitengo cha Itelijensia wa TANAPA Emil
Kisambo.
Wengine ni Mkuu wa Hifadhi ya Serengeti Mtango Mtaiko na Mratibu wa Mradi wa Faru Serengeti Nyafuru Nyamafumbati.
Pamoja na hao pia watumishi wengine28 wameandikiwa barua za kusimamishwa kazi ili kupisha uchunguzi wa tukio hilo.
Chanzo:- www.dewjiblog.com


إرسال تعليق