Na Khadija Mngwai
MSHAMBULIAJI ‘denja’ wa Simba, Emmanuel Okwi (pichani), amesema
pamoja na mapenzi yake makubwa kwa timu hiyo lakini yupo tayari kujiunga
na Azam.
Okwi, raia wa Uganda, amesema yupo tayari kujiunga na Azam
FC ambayo pia itashiriki michuano ya kimataifa baada ya kushika nafasi
ya pili katika Ligi Kuu Bara msimu huu.
Azam walianza kumsaka Okwi
tangu msimu uliopita lakini juhudi zao zikagonga mwamba ingawa
walifanikiwa kumpata beki mwingine kisiki wa zamani wa Simba, Joseph
Owino.
Owino na Okwi walitua nchini pamoja na kujiunga na Simba, misimu mitatu iliyopita.
Akizungumza
na Championi Jumatano, Okwi alisema hawezi kukataa ofa yoyote
itakayopelekwa kwake na Azam, hasa kama ataona ina maslahi kwake na pia
kwa Simba.
“Hadi sasa bado sijapata ofa yoyote kutoka Azam wala
katika timu yoyote, nimekuwa nikisikia tu kutoka kwenye vyombo vya
habari, lakini mimi ni mchezaji, nipo tayari kuondoka Simba iwapo ofa
yoyote itakuja kwa maslahi.
“Klabu yoyote ikinifuata kutaka kunisajili msimu ujao itakuwa faida kwangu na kwa Simba kwa jumla.
“Kwa
sasa bado nina mkataba na klabu yangu ya Simba, hivyo timu
itakayonihitaji ni lazima ivunje mkataba kulingana na makubaliano,”
alisema Okwi.
Tayari Azam FC ilishaanza mazungumzo kimya kimya na
Simba, mara ya mwisho ‘Lambalamba’ waliahidi kutoa kitita cha Sh milioni
50 pamoja na Mrisho Ngassa ili wapewe Okwi.
Lakini taarifa zinaeleza
kuwa, uongozi wa Simba ‘ulitoa nje’ ingawa nao ulikuwa ukiwabembeleza
Azam FC umpate Ngassa kwa kuwa alikuwa pendekezo la Kocha Mkuu, Milovan
Cirkovic.
Milovan anataka kumtumia Ngassa kama kiungo mshambuliaji wa
kulia na Okwi kushoto huku Haruna Moshi ‘Boban’ akigonga namba ‘ten’ na
Sunzu anamaliza kati, yaani tisa.
Chanzo: GPL

إرسال تعليق