Shirika
la Umeme Tanzania (Tanesco), linahitaji Sh. tilioni 1.3 kwa ajili ya
kuboresha miundombinu ya usambazaji wa umeme katika maeneo mbalimbali ya
nchi.
Kadhalika,
Tanesco limetangaza kuwa hali ya maji katika mabwawa yake ya kuzalisha
umeme ni mbaya na kwamba kama litategemea chanzo hicho pekee uzalisjhaji
utasitisha ifikapo Agost mwaka huu.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Tanesco, William Mhando, aliyasema hayo jana jijini Dar es
Salaam alipozungumza
na waandishi wa habari. Alisema ikiwa serikali itawasaidia kiasi hicho cha fedha wataweza kuimarisha miundombinu ya usambazaji wa umeme na hivyo kusaidia kupata umeme wa uhakika.
na waandishi wa habari. Alisema ikiwa serikali itawasaidia kiasi hicho cha fedha wataweza kuimarisha miundombinu ya usambazaji wa umeme na hivyo kusaidia kupata umeme wa uhakika.
Alisema
miundombinu ya nguzo na mitambomingine imechoka na kwamba hatua hiyo
imetokana na serikali kuliacha shirika hilo kwa muda mrefu bila kuweka
fedha wakati ilipokuwa ikisubiri kulibinafsisha.
Aidha,
Mhando alisema mchakato wa kupata mkopo wa Sh. bilioni 408 umefikia
hatua za mmwisho na kwamba muda wowote fedha hizo zitatolewa.
Kuhusu hali ya maji katika mabwawa mbalimbali hapa nchini, Mhando alisema kina chake kimepungua.
Bwawa la Mtera alisema kina cha juu cha maji kinachotakiwa ili
kuzalisha umeme ni ujazo wa mita 698.5 kutoka usawa wa bahari na cha
chini ni mita za ujazo 690 kutoka usawa wa bahari.
Alisema
kwa sasa bwawa hilo lina ujazo wa mita 691.36 kutoka usawa wa bahari na
kwamba kimeabaki kiasi kidogo kufikiwa ili kusitisha uzalishaji wa
umeme katika chanzo hicho. “Bwawa likifikia mita za ujazo 690 kutoka
usawa wa bahari inatakiwa uzalishaji wa umeme usitishwe ama tupate
kibali maalum cha serikali,” alisema.
CHANZO:
NIPASHE
إرسال تعليق