Timu ya kikapu ya Andi 1 yang'ara katika ziara yake,Wapagawa katika tamasha la Coca Cola A Billion Reasons to Believe

Timu ya kikapu ya Andi 1 yang'ara katika ziara yake,Wapagawa katika tamasha la Coca Cola A Billion Reasons to Believe

Mchezaji wa And 1 akifunga katika mechi dhidi ya kombaini ya mkoani Arusha
Mchezaji wa And 1 Chism akipaa hewani kufunga dhidi ya Dar es Salaam
 Mwanamuziki Nemless kutoka nchini Kenya akitumbuiza katika tamasha hilo.
Mwanamuziki Ambwene Yesaya AY akifanya viti vyake katika tamasha hilo.


 Na Mwandishi wetu
  Timu ya mpira wa kikapu inayoundwa na wachezaji nyota wa zamani wa ligi ya Chama mpira wa kikapu cha Marekani American Basketball Association (ABA)  ijulikanayo kwa jina la AND1 imemaliza ziara yake kwa mafanikio makubwa huku ikiacha somo na gumzo kwa Watanzania kutokana na ujuzi walionyesha katika mchezo huo.
 
Andi 1 iliyokuwa chini ya mchezaji nyota, Dennis Chism maarufu kwa jina la Spyda iliweza kufanya mambo makubwa mkoani Mwanza na Arusha baadaye jijini Dar es Salaam na kuitandika Dar Dream team kwa 123-71.
 
Mbali ya Spyda, wachezaji wengine waliokuwepo katika ziara hiyo ni Phillip Champion Hotsauce, Robert Martin, Marvin Collins Highrizer, Brandon LaCue Werm, Jamar Davis, Alonzo Miles, Paul Otim na Justin Darlington.
 
Chism alisema pamoja na kuwashukuru wauzaji wa kinywaji cha Sprite kwa udhamini wao na kufanikisha kuja nchini, wamefuraishwa na jinsi wachezaji wa Tanzania waliovyoonyesha vipaji vyao. Alisema kuwa wachezaji hao wanatakiwa kuendelezwa ili kufikia hatua kubwa na hata kuweza kucheza ligi za kikapu za kulipwa Duniani pamoja na ile ya NBA.
 
Mbali ya kucheza, wachezaji hao walionyesha vipaji mbali mbali walivyonavyo katika kufunga pointi tatu, ku-dank na staili nyingine ambazo ziliwasisimua mashabiki wengi.
 
Baada ya kushiriki katika mechi za mpira wa kikapu, wachezaji hao walijumuika na watanzania wengine katika tamasha la muziki la Coca Cola A Billion Reasons to Believe lililofanyika kwenye  ufukwe wa Mbalamwezi na kuona jinsi gani watanzania walivyokuwa wataalam katika muziki wa kizazi kipya na hip hop ambao asili yake ni Marekani ambako wao ndiyo maskani yao.
Wakali wa muziki kama Ambwena Yesaya (AY) na Nemeless kutoka Kenya walitamba katika tamasha hilo lililofana na kuwavutia mashabiki wengi

Post a Comment

Previous Post Next Post