WANANCHI WAMUOMBA MKUU WA MKOA KUTATUA MGOGORO WA KUTENGULIWA MWENYEKITI WA KIJIJI - MBEYA
Wananchi
wa Kijiji cha Ijumbi, Kata ya Ruiwa Wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya,
wamemuomba Mkuu wa Mkoa Bwana Abbas Kandoro kuingilia kati mgogoro baina
ya pande mbili zinazopingana Diwani na Afisa Mtendaji wa Kata wakidaiwa
kumuengua Mwenyekiti wa kijiji hicho kwa kutumia madaraka yao.
Kauli
hiyo imetolewa na wananchi wa Kata hiyo kawa nyakati tofauti wakati
wakiongea na mtandao huu kijijini hapo, ambapo inadaiwa Mwenyekiti wa
Kijiji hicho Bwana John Kalikumoyo ameenguliwa uongozi kutokana na
ubadhilifu pia kuitisha mikutano ya hadhara bila kibali na kuzuia
wananchi katika shughuli za maendeleo.
Wananchi
hao wamepinga madai hayo na kuwa ni njama za mtendaji Kata Bwana Jordan
Masweve na Diwani mheshimiwa Alex Mdimilage, kwani ya kudhoofisha
juhudi za mwenyekiti huyo kwa kuzuia mianya ya upatikanaji wa pesa
kinyume na utaratibu wa makusanyo ya pesa za serikali.
Imedaiwa
kuwa Viongozi hao wa kata waliitisha mkutano wa halmashauri ya Kijiji
Aprili 17 mwaka huu, wakimtuhumu Bwana Kalikumoyo kwamba ameuza ng'ombe
aliyekamatwa kijijini hapo na kujipatia fedha jumala ya shilingi milioni
1,080,000 na makosa hayo yanafanya kupoteza sifa za kuwa kiongozi.
Aidha
viongozi hao walimtaarifu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya
Mbarali na yeye kuandika barua Aprili 18 mwaka huu, kutengua uongozi wa
uenyekiti wa kijiji na kumkaimisha Afisa Mtendaji wa Kijiji.
Katika
sakata hilo wananchi wa kijiji hicho wamemuomba Mkuu wa Mkoa Bwana
Kandoro, kwenda haraka iwezekanavyo kijijini hapo ili kuleta suluhu
kwani wananchi hao wamedai kuwa viongozi hao wa kata Bwana Masweve na
Mdimilage ndio wabadhilifu.
Hata
hivyo miongoni mwa vitendo vinavyolalamikiwa na wanachi kwa viongozi
hao ni pamoja na kujipatia zaidi ya shilingi milioni 24 kutoka kwa
wafugaji ambazo hazijaingia katika mfuko wa kijiji, ba kwamba suala hili
Mkuu wa mkoa anapaswa kuunda tume ya kuchunguza kwani hawapo tayari
kuchangia shughuli za maendeleo kama vile ujenzi wa shule za sekondari,
zahanati na maji.
Wakati
huo huo wamesema sababu yao ya kutka kususia kuchangia shughuli za
maendeleo ni kutokana na viongozi hao kukataa kusoma bajeti ya mapato na
matumizi ya kijiji, na badala yake kuwataka viongozi wa Vijiji kusoma
taarifa hizo, hali inayowapelekea kuwa na swali kuwa Serikali ya kata
haina mapato na matumizi?.
Chanzo:- Mbeya Yetu
Post a Comment