Ujumbe toka Afrika, Mashariki ya Kati na Ghuba ya Uajemi wawasili Marekani
Ujumbe toka Afrika, Mashariki ya Kati na Ghuba ya Uajemi ukiongozwa
na Rais wa IBF-Africa Mtanzania Onesmo Ngowi umewasili katika uwanja wa
ndege wa Oahu, jiji la Honolulu, Hawaii na kulakiwa na Mstahiki Meya wa
jiji la Hawaii Peter Carlisle.
Ujumbe huo unajumuisha wawakilishi toka Afrika ya Kusini, Botswana,
Uganda, Ghana, Nigeria, Oman, UAE (Dubai), Jordan, Gabon, Morocco,
Ivory Coast na Tanzania.
Jana, ujumbe huo ulifanya mazungumzo na Mstahiki Meya wa jiji la
Los Angelos, Antonio Villaraigosa katika chumba cha watu mashuguri (VIP)
kwenye uwanja wa ndege wa Los Angelos na kuzungumzia masuala ya Utalii
katika Afrika, Mashariki ya Kati na Ghuba ya Uajemi.
Meya Villaraigosa aliahidi kuwahamasisha watu wa Los Angelos
kutembelea na kuwekeza katika ukanda huu na kuukaribisha ujumbe huo
kulitembelea jiji la Los Agelos mwezi wa tida kwaka huu.
Wajumbe toka Botswana, Afrika ya Kusini, Oman, Jordan na UAE (Dubai) wamefuatana na wafanyabishara wa Utalii (Tour Operators).
Mkutano mkuu wa IBF/USBA utafanyika katika hotel ya Hawaii Hilton
Village katika mji mdogo wa Waikiki, jiji la Honolulu, Hawaii, Marekani.
Huu ni mkutano unaohudhuriwa na wajumbe zaidi ya 6000 toka nchi 204
duniani.
Hawii Hilton Village ipo kwenye eneo la hekari 28 ambapo kuna
majengo na maduka makubwa ya bidhaa mbalimbali. Hapa ndipo IBF itafanya
mkutano wake wa mwaka wa 29. Hapa ndipo ujumbe toka Afrika, Mashariki ya
Kati na Ghuba ya Uajemi utatoa mpango wake wa Utalii wa Michezo (Sporst
Tourism).
Ujumbe wa bara la Afrika, Mashariki ya Kati na Ghuba ya Uajemi uko
hapa kutangaza biashara ya utalii ili kuweza kuwanasa watalii wengi
wanaotoka sehemu mbalimkbali duniani na wanaohudhuria kwenye mkutano
huu. Mkutano huu utaanza rasmi tarehe 29 Juni, 2012.
Jimbo la Hawaii linajulikana kwa wengi kutokana na umaarufu wake
katika vita vya pili vya dunia wakati Wajapani na Manazi waliposhambulia
Pearl Habor mwaka 1941 ambapo iliilazimu Amerika ambayo kwa wakati huo
ilikuwa haina upande (Neutral) kujiunga na vita ya pili ya dunia ambapo
baadaye ilimalizika!

إرسال تعليق