Wazazi
watakaoshindwa kuwapeleka shule watoto wao nchini Kenya watakuwa katika
hatari ya kuhukumiwa kifungo cha jela iwapo mswada mpya uliowasilishwa
utapitishwa kuwa sheria.
Mswada huo unapendekeza mzazi kupigwa faini ya shilingi 5,000 ya Kenya au kufungwa jela kwa muda wa mwaka mmoja.
Katika
hatua nyingine mitihani ya majaribio itazuiliwa na hakuna mwanafunzi
atakayenyimwa kuingia katika shule yeyote ya msingi ya serikali.
Hata
hivyo mwanafunzi yeyote atayeshindwa kuendana na utaratibu wa shule
kutokana na sababu za kiakili, kimaumbile au kisaikolojia anaweza
kuondolewa kwa kibali cha Waziri wa Elimu.
Mswada huo uliochapishwa na Waziri wa Elimu Mutula Kilonzo umeandaliwa baada ya kufanyika kwa mfululizo wa mashauriano.
Kwanza
wizara ya elimu iliunda kikosi kazi chini ya Makamu wa Rais wa Chuo
Kikuu cha Moi Profesa Douglas Odhiambo, ambacho kiliandaa ripoti ambayo
ilipitiwa katika mkutano wa kitaifa wa wadau wa elimu uliofanyika mwezi
Machi jijini Nairobi.

إرسال تعليق