Meneja
Mkuu wa Kampuni ya Global Publishers, Abdalah Mrisho (wa pili kushoto)
akiwa na wajumbe wenzake wa Kamati ya Maandalizi ya mkutano huo,
wakiandaa mazingira kabla ya mkutano huo kuanza. Wa kwanza kulia ni Bi.
Joyce Mhavile wa ITV/Radio One, anayemfuatia ni Masoud Sanani wa
Business Times na wa kwanza kushoto ni Hamza Kasongo wa Channel Ten.
Mwenyekiti
Mtendaji wa Makampuni ya IPP na Mwenyekiti wa Chama Cha Wamiliki wa
Vyombo vya Habari nchini (Moat), Reginald Mengi, akifungua mkutano huo.
Waziri
wa Habari, Utamaduni na Michezo, Dk. Emmanuel Nchimbi, akitoa hotuba na
kuwasifu wamiliki wa vyombo vya habari nchini kwa kuamua kwa hiyari yao
kuanzisha muungozo huo.
Waziri
Nchimbi akiweka saini makubaliano hayo na Mwenyekiti wa Moat, Reginald
Mengi (kulia) na Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya kuendeleza Vyombo vya
Habari Afrika (AMI), Amadou Mahtar Ba.
Wakijadiliana jambo baada ya kutiliana saini makubaliano hayo.
Waziri Nchimbi na Mengi wakiwa na nyuso za furaha wakati wakiteta jambo.
Mwenyeki wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, akichangia mada wakati wa mjadala wa kuboresha taaluma ya habari.
Mwanasiasa maarufu nchini, Prince Bagenda naye akichangia hoja.
Wajumbe
wa Kamati ya Maandalizi ya uzinduzi wakiwa katika picha ya pamoja.
Kutoka kulia, Henry Muhanika (Katibu), Masoud Sanani (Mjumbe), Abdallah
Mrisho (Mjumbe), Theophil Makunga (Mwenyekiti) na Hamza kasongo
(mjumbe).
Mwenyekiti wa Moat, Reginald Mengi, akiongea na wanahabari baada ya kutiliana saini makubaliano hayo.
Ulipowadia wakati wa maakuli.
Wamiliki na mameneja wa vyombo vya habari nchini leo wametiliana
saini mbele ya Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo, Dkt. Emmanuel
Nchimbi, makubaliano ya hiyari ya kuanzisha na kulinda Muungozo na
kanuni za kuendesha vyombo vya habari nchini na nchi zingine barani
Afrika. Makubaliano hayo yalisainiwa kwenye mkutano wa uzinduzi
uliofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Katika mkutano
huyo mijadala mbalimbali ya kuboresha taaluma ya habari ilijadiliwa.
Chanzo:- globalpublishers
إرسال تعليق