Kocha mkuu wa zamani wa timu ya taifa ya England
Sven-Goran Eriksson anasema wanaomshtumu kocha wa sasa Roy Hodgson kwa
kutomchagua Rio Ferdinand kwenye timu wana nia ya kumchafulia jina.
Ferdinand hakuwepo kwenye kikosi cha kwanza
kilichotajwa na kocha Roy Hodgson na wakati Gary Cahill alipopata
jeraha, kocha huyo alimuita Martin Kelly mwenye umri wa miaka 22.
"
Kumchagua Kelly inaonekana kumemponza," Eriksson alisema. "kwa kuwa
amechagua wachezaji sita wa Liverpool, Roy sasa anaandamwa.
" Najua Roy atakabiliana na hali hiyo bila wasiwasi wowote."
Hodgson, ambaye tayari ameiongoza timu hiyo
kupata ushindi katika mechi mbili za kirafiki tangu kuchukua uongozi wa
timu ya England mwezi uliopita, amesisitiza kuwa kuachwa nje kwa
Ferdinand ni kwa sababu za kimchezo wala siyo vinginevyo.
Hata hivyo wengi wanaamini ni kwa nia ya kuepuka
matatizo kati yake na John Terry, ambaye anatarajiwa kufika mahakamani
mwezi ujao kwa tuhuma za kumrushia maneno ya ubaguzi wa rangi mdogo wake
Ferdinand, Anton, tuhuma ambazo nahodha huyo wa Chelsea,Terry
anakanusha.
إرسال تعليق