TAARIFA MBALIMBALI KUTOKA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TFF
KIINGILIO MECHI YA TAIFA STARS, GAMBIA 3,000/-
Kiingilio
cha chini ya mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia kati ya Tanzania (Taifa
Stars) na Gambia (The Scorpions) itakayochezwa Jumapili (Juni 10 mwaka
huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ni sh. 3,000.
Watazamaji
watakaolipa kiingilio hicho ni watakaokaa kwenye viti vya rangi ya bluu
na kijani ambavyo ni 36,693 kati ya jumla ya viti 57,558 vilivyopo
katika uwanja huo wa kisasa. Kiingilio kwa viti vya rangi ya chungwa ni
sh. 5,000.
Kwa
upande wa VIP C watalipa sh. 10,000 wakati VIP B ni sh. 20,000.
Kiingilio kwa jukwaa la VIP A ambalo linachukua watazamaji 748 tu ni sh.
30,000 kwa mechi hiyo itakayoanza saa 10 kamili jioni.
Tiketi
zitaanza kuuzwa Jumamosi (Juni 9 mwaka huu) kuanzia saa 2 asubuhi
kwenye vituo vya Mgahawa wa Steers ulioko Mtaa wa Ohio na Samora, Shule
ya Sekondari Benjamin Mkapa, Soko Kuu la Kariakoo na Uwanja wa Taifa.
Siku ya mechi pia mauzo yatafanyika katika vituo hivyo na baadaye
kuhamia Uwanja wa Taifa.
إرسال تعليق