JK Akutana Na Wabunge Wa Afrika Mashariki


THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

Telephone: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: ikulumawasiliano@yahoo.com
press@ikulu.go.tz
Fax: 255-22-2113425

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Jakaya Mrisho
kikwete, mchana huu Juni 4, 2012 amekutana na Wabunge wa Tanzania
katika Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki jijini Arusha.

Mhe. Rais, ambaye aliwakaribisha Wabunge hao kwa chakula cha mchana
katika hoteli ya Ngurdoto Mountain Lodge, aliwapongeza kwa kuchaguliwa
kwao kuiwakilisha Tanzania katika Bunge hilo la Jumuiya, na kuwataka
wasimamie na kutetea maslahi ya nchi wakiwa huko.

Pia Rais amewataka Wabunge hao kuwa karibu na Serikali katika
kushauriana namna ya kukabiliana na changamoto zitazojitokeza katika
kazi zao, na kuwakumbusha kwamba majukumu ya Bunge hilo la Jumuiya
ni kusimamia makubaliano (treaty) yaliyoyoorodheshwa katika kuundwa
kwake na kuendeshwa.

Alisema: “Msome vyema na kuyaelewa makubaliano (treaty) hayo yote na
vipengele vyake na msaidie kuiendeleza Jumuiya ambayo wanachama
wote watanufaika nayo, na siyo upande mmoja.

“Tumewapeleka pale kwa ajili ya maslahi ya Tanzania hivyo mjue kuna
kazi nyingi kweli, hasa katika kujadili yale yote yaliyokubaliwa katika
makubaliano ya jumuiya” alisema.

Mhe. Rais alikutana na Wabunge wote wa Tanzania katika Bunge la
Jumuiya ya Mashariki isipokuwa mmoja, Bi. Nderkindo Perpetua Kessy
ambaye hakufika kwa sababu iliyoelezwa kuwa ni mgonjwa.

Waliofika ni pamoja na Mwenyekiti wa Wabunge wa Tanzania kwenye
Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki, Alhaj Adam Omar Kimbisa na
Katibu wake, Mh Shy-Rose Saddrudin Bhanji.

Wengine waliofika ni Mhe. Anjela Charless Kizigha, Mh. Maryam Ussi
Yahya, Dkt Twaha Issa Taslima, Mhe. Abdullah Ali Hassan Mwinyi, Mhe
Bernard Musomi Murunya na Mhe. Charles Makongoro Nyerere.

Wabunge hao wanatarajiwa kuungana na wabunge wenzao wa Kenya,
Uganda, Rwanda na Burundi kesho Juni 5, 2012 katika kikao chao rasmi
cha kwanza ambapo watamchagua Spika na kasha kula viapo kabla ya
kuanza majukumu yao.

..……..Mwisho……….

Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

Ikulu.

DAR ES SALAAM.

Post a Comment

أحدث أقدم