MECHI ya hisani kati ya Simba na APR ya Rwanda ya kuichangia familia
ya aliyekuwa kiungo wa kimataifa wa Rwanda, Patrick Mutesa Mafisango
aliyefariki Aprili 17, itachezwa Julai 8, kwenye Uwanja wa Taifa, jijini
Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga, uhakika wa mechi
hiyo umetokana na kufahamika kwa tarehe ya kuanza michuano ya Klabu
Bingwa Afrika Mashariki na Kati (Cecafa).
“Mechi ya hisani itachezwa Julai 8 kwenye Uwanja wa Taifa kwani tayari
tumeshajua tarehe ya kuanza kwa michuano ya Kombe la Kagame,” alisema
Kamwaga na kutoa wito kwa wapenzi wa soka kumuenzi nyota huyo kwa kufika
uwanjani siku hiyo.
Aidha, klabu ya Simba imeweka kibao cheusi kwenye mti uliopo eneo la
ajali iliyogharimu uhai wa nyota huyo, kikiwa na maneno yasemayo ‘Burian
Mafisango’ na tarehe ambayo ajali hiyo ilitokea.
Kamwaga alisema kwa sasa wanafuaatilia kibali Manispaa ya Temeke
wakitaka kuweka alama mahali hapo na kusema, kibao hicho kimewekwa na
marafiki zake wa mtaani kwake, Chang’ombe

إرسال تعليق