MAJERUHI WAONGEZEKA STARS, KIM POULSEN AELEZA MIKAKATI YA KUUA MAMBA
Kim Poulsen |
KOCHA Mkuu wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa
Stars, Mdenmark Kim Poulsen amesema kwamba kipa Mwadini Ally na beki Waziri
Salum wameingia kwenye orodha ya wachezaji majeruhi katika kikosi chake, wakati
akijiandaa na mechi dhidi ya Msumbiji, ‘Mambas’ kuwania tiketi ya kucheza
Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwakani Afrika Kusini.
Stars ambayo itacheza na Mambas Juni 17, mwaka huu kwenye
Uwanja wa Taifa, Zampeto nje kidogo ya Jiji la Maputo kuanzia saa 9 mchana kwa
saa za huko, mechi ya kwanza ilitoka sare ya 1-1 na Msumbiji, Dar es Salaam na
katika mchezo huo inatakiwa lazima ishinde au itoke sare ya zaidi 2-2 ifuzu kwa
faida ya bao la ugenini.
Akizungumza na Waandishi wa Habari mchana wa leo leo, ofisi za
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Poulsen amesema maandalizi ya kikosi chake
yanakwenda vizuri ingawa Mwadini Ali na Waziri Salum wameungana na Naasor Masoud
‘Chollo’ katika ‘meza ya majeruhi’ na hawatakuwemo kwenye msafara wa timu hiyo
utakaoondoka Juni 15 mwaka huu saa 11 alfajiri kwa ndege ya Kenya Airways
kupitia Nairobi.
Kocha huyo amesema baada ya mechi tatu maendeleo kiuchezaji
kwa timu yake inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager ni mazuri ingawa bado
anafanyia kazi kwa nguvu safu ya ushambuliaji. Mechi iliyopita Taifa Stars
iliifunga Gambia 2-1 huku mabao yote yakifungwa na mabeki.
Iwapo Taifa Stars itaitoa Msumbiji katika raundi ya mwisho
itapangiwa moja kati ya timu 16 zilizocheza Fainali za AFCON zilizofanyika
Januari mwaka huu katika nchi za Gabon na Equatorial Guinea. Katika mechi ya
kwanza dhidi ya Msumbiji iliyochezwa Dar es Salaam, Februari 29 mwaka huu timu
hizo zilitoka sare ya bao 1-1.
Taifa Stars ambayo msafara wake utakuwa na wachezaji 20
itaagwa kesho (Juni 14 mwaka huu) saa 6 mchana kambini kwao- hoteli ya
Accommondia (Tansoma) jijini Dar es Salaam.
Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) kwa ajili ya kujenga
afya kupitia mpira wa miguu.
Post a Comment