RAMANI NA VIPIMO VYA UWANJA WA SOKA!

RAMANI NA VIPIMO VYA UWANJA WA SOKA!

Wengi tunaupenda mchezo wa soka lakini je sheria zenyewe zinazoongoza mchezo huu tunazifahamu? blog yako inakuletea sheria za mchezo huu, hii ni kwa ajili ya kuwafanya wasomaji wetu nanyi mfahamu sheria 17 za mchezo huu.

SHERIA YA 1:UWANJA WA MICHEZO
1: vipimo

  Kiwanja cha michezo  kina umbo la  mstatili. Urefu wake
hautazidi yadi 130 na hautapungua yadi 110. Upana wake
hautazidi yadi 100 wala hautapungua yadi 50. Kiwanja cha michezo ya kitaifa urefu hautazidi yadi 80 wala kupungua yadi 110, na upana hautazidi yadi 80 wala kupungua yadi 110, na upana hautazidi yadi 80 wala kupungua yadi 70. Kwa vyovyote vile, marefu yatazidi mapana.

2: Alama

Mistari inayoonekana wazi, yenye unene usiozidi inchi 5
itachorwa kuonyesha mipaka ya kiwanja. Mistari ya urefu
itaitwa mistari ya pembeni na ile ya mapana, itaitwa mistari ya goli.

Bendera iliyootundikwa kwenye mti usiopungua futi 5 kwa urefu itasimikwa katika kila kona  ya kiwanja. Bendera ya aina hii yaweza kusimikwa sawa na mstari wa kati umbali usiopungua yadi moja kutoka mstari wa pembeni. Mstari wa katikati utapita katikati ya kiwanja na alama itawekwa
kuonyesha katikati ya kiwanja na alama itawekwa kuonyesha katikati kabisa. Kutoka kwenye alama hiyo,mnviringo wenye nusu kipenyo  cha
yadi 10 utachorwa. Alama hiyo ya kati ndipo mahali pa kuanzia michezo.


3: Eneo la goli
Katika kila upannde wa goli mistari miwili itachorwa pembe mraba na mstari wa goli. Eneo lililomo ndani  ya mistari hii litajulikana kama eneo la goli.

4: Eneo la Adhabu
Katika kila upande wa goli mistari miwili itachorwa pembe
mraba na mstatiri wa goli umbali wa yadi 18 toka kila nguzo  ya goli. Mistari hii itaingia uwanjani umbali wa yadi 18 na itaungwa kwa mstari wa usawa na ule wa goli. Eneo hili litajulikana kama eneo la adhabu. Alama itawekwa umbali wa yadi 12 kutoka katikati ya mstari wa goli, na hapo ndipo pa kupiga penalti. Kutoka alama hiyo
mkato wenye nusu kipenyo cha yadi 10 utachorwa nje ya eneo la adhabu.


5: Eneo la kona
Robo ya mviringo yenye nusu kipenyo cha yadi itachorwa ndani ya kiwanja kutoka mahali ilipo bendera ya kona. Eneo hili ndio eneo la kona.

6: Magoli
Nguzo za goli zitasimikwa katikati ya mistari ya goli, zikiacha urefu sawa toka kila kona. Umbali kati ya nguzo na nguzo utakua yadi 8. Juu ya nguzo kutawekwa mwamba na urefu wa ndani ya gali toka chini hadi hadi juu, mwamba huo hautazidi inchi 5.
Baraza la michezo la mataifa  FIFA  limeamua katika sheria katika sheri hii ya kwanza ya mchezo wa soka
kwamba;

1: Vipimo vya kiwanja cha mchezo wa kimataifa vitakuwa; si zaidi ya yadi 120 +  80 wala si chini ya yadi 100 + 70. (Wastani
m105 + m70)
Chanzo:- Shaaffihdauda blog

Post a Comment

Previous Post Next Post