MATREKTA madogo aina ya ‘Power tiller’ yaliyonunuliwa na baadhi
ya wakulima wa Kijiji cha Kisaki wilayani Morogoro, yamegeuzwa kuwa
magari ya kubeba wagonjwa hususan akina mama wajawazito.
Baadhi ya wakazi wa kijiji hicho, walisema hayo jana mjini hapa wakati
wakitoa mrejesho juu ya masuala yanayorudisha nyuma maendeleo kwa jamii
kwenye mkutano uliowakutanisha wananchi na viongozi wa serikali
wilayani hapa.
Wanakijiji hao walidai kuwa, kutokana na kuharibika kwa miundombinu,
wananchi wengi na hasa wajawazito, hufa kwa kukosa huduma, jambo
lililowafanya kuamua kugeuza matrekta hayo kuwa magari ya wagonjwa, na
kuwapeleka katika Kituo cha Afya Duthumi, kilomita zaidi ya 40.
Mmoja wa wakazi hao, Tatu Maleta, alidai kuwa pamoja na umuzi huo,
bado wagonjwa wengi hufia njiani na akina mama kujifungua kabla ya
kufika katika zahanati kwa sababu matrekta hayo yamekuwa yakitembea
polepole.
Wanakijiji hao walisema pia huduma za maji, elimu, ukosefu wa masoko
zimendelea kuwa duni kila kukicha, huku usafiri wa kutoka nje ya kijiji
hicho wakitegemea zaidi basi moja dogo aina ya Coaster.
Chanzo:- Tanzania daima
إرسال تعليق