Andy Murray, mchezaji bora zaidi wa kiume katika
mchezo wa tennis nchini Uingereza, amefanikiwa kuingia robo fainali,
baada ya kumshinda Richard Gasquet wa Ufaransa katika mashindano ya
French Open, uwanja wa Roland Garros.
Murray, ambaye amepangwa kama mchezaji wa nne
bora zaidi katika orodha ya wachezaji mahiri katika mashindano hayo ya
Ufaransa, alilemewa katika seti ya kwanza, na inaelekea maumivu ambayo
yalikuwa yanamharibia mapambano yake ya awali yalikuwa yamembana tena.
Hata hivyo aliweza kujikakamua na kupata ushindi katika seti ya pili, kabla ya kumuondoa Gasquet kwa 1-6 6-4 6-1 6-2.
Murray sasa Jumatano atapambana na David Ferrer wa Uhispania katika kujitahidi kuingia nusu fainali.
إرسال تعليق