Kundi moja la wapiganaji wakiwa silaha kali
wamedhibiti barabara ya ndege katika uwanja wa ndege jiji kuu la
Tripoli, Libya. Waasi hao wamekuwa wakitaka kuachiliwa kwa kiongozi wao
wanaodai alikamatwa Ijumaa wiki jana.
Kundi hilo la al-Awfia brigade liliingia katika
uwanja wa ndege hali iliyolazimisha ndege nyingi kubadilisha safari.
Haijabainika ikiwa kiongozi wa kundi hilo anazuiliwa na serikali ili
kuhojiwa.
Wapiganaji hao wamepinga kuondoka
uwanja huo hadi masharti yao yatekelezwe.Makundi ya wapiganaji wakiwa na silaha kali wangali kwenye uwanja
huo.
Rubaa zaidi zinasema baadhi ya maafisa wamekuwa
wakiwasihi wapiganaji hao kuondoka eneo hilo.Magari kadhaa ya kijeshi
yamefika katika uwanja huo.
Mmoja wa waakilishi kutoka eneo linalodhibitiwa
na wapiganaji hao la Tarhouna magharibi mwa Libya amekuwa akishauriana
na waasi hao ili kuondoka uwanja wa ndege.
Duru katika uwanja wa ndege zinasema kampuni
tatu za ndege zimefuta safari zake.Safari kadhaa za kimataifa
zimerejesha huduma zake nchini Libya baada ya amani kurejea kufuatia
mapigano ya kumuondoa madarakani Kanali Muammar Gaddafi.
Serikali ya Libya ilichukua udhibiti wa uwanja
wa ndege kutoka kwa wapiganaji ambao wamekuwa wakilinda uwanja wa ndege
kwani hakuna kikosi rasmi cha jeshi la polisi.
إرسال تعليق