WABUNGE walio katika Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma,
wanakusudia kumsulubisha tena aliyekuwa Waziri wa Fedha, Mustafa Mkulo
kutokana na tuhuma alizozitoa bungeni kwamba wajumbe hao wamehongwa
kuhusiana na suala la Shirika Hodhi la Mashirika ya Umma (CHC).
Mkulo ni kati ya mawaziri walioachwa katika mabadiliko ya Baraza la Mawaziri yaliyofanywa mwanzoni mwa mwezi Mei mwaka huu na Rais Jakaya Kikwete baada ya kuwapo kwa tuhuma za ufisadi uliobainishwa kupitia ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).
Katika Mkutano wa Nne wa Bunge, Mkulo aliituhumu Kamati hiyo kwamba walihongwa ili kutetea nyongeza ya muda wa CHC, tofauti na mawazo ya Serikali ya kutaka kufutwa kwa shirika hilo.

Baada ya tuhuma hizo, Mwenyekiti
wa POAC, Zitto Kabwe aliapa bungeni kwamba kama uchunguzi utathibitisha
yeye au wajumbe wake wamehongwa, angejiuzulu uenyekiti na ubunge na
kumtaka Waziri Mkulo nae atoe kiapo chake bungeni kama atajiuzulu
akibainika amefanya ufisadi ndani ya CHC.
Mkulo akijibu swali hilo alishindwa kula kiapo na Spika wa Bunge, Anne Makinda akamkumbusha kuhusu kula kiapo kama atajiuzulu, lakini waziri huyo aligoma kufanya hivyo.
Lakini jana baadhi ya wajumbe wa POAC ambao ni wabunge wa CCM na wale wa upinzani waliliambia gazeti hili kwa nyakati tofauti kwamba Mkulo aliwadhalilisha kwa kuwatuhumu kwamba walipokea rushwa, hivyo watamtaka athibitishe kauli yake au hatua za kinidhamu zichukuliwe dhidi yake.
“Hatuwezi kukaa kimya kuhusu suala hili maana alitukosesha rah asana kwa kututuhumu kwamba tumepokea rushwa, hebu fikiri kama tuhuma hizo zingetolewa na mbunge wa kawaida tu dhidi ya Waziri ingekuwaje? Lazima tushughulikie jambo hili tena katika kikao cha Bunge la Bajeti,”alisema mmoja wa wabunge wa CCM ambaye ni mjumbe wa POAC.
Mbunge mwingine wa upinzani aliliambia gazeti hili jana kwamba suala la kumbana Mkulo ili achukuliwe hatua za kinidhamu halina itikadi na kwamba watahakikisha wanatumia kanuni za Bunge kumfikisha mbele ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge ili ajibu tuuma za kusema uwongo bungeni.

Kauli za wabunge hao, zinafanana na ile
iliyotolewa na mbunge mwenzao wa CCM juzi alipoliambia gazeti hili
kwamba suala la Mkulo kuwatuhumu wajumbe wa POAC kwa rushwa haliwezi
kupita bila wajumbe hao kusafishwa ndani ya Bunge.
Mwenyekiti wa POAC Zitto Kabwe akizungumza jana kwa simu alisema: “Mimi kwangu Mkulo kwa sasa si jambo muhimu kwasababu tayari tuna Waziri mwingine wa Fedha na Uchumi ambaye nadhani tunatakiwa kumbana ili tupate bajeti nzuri kwa ajili ya maendeleo ya nchi yetu na wananchi wetu kwa ujumla”.
Aliongeza: “Hata hivyo kama wajumbe wa POAC wanadhani walidhalilishwa kwa kauli hiyo ya mheshimiwa Mkulo, mimi nadhani wana haki ya kutumia taratibu za kibunge kulishughulikia ili kanuni zetu za Bunge zichukue nafasi yake”.
Zitto alisema ikiwa suala hilo litafikishwa mbele Kamati ya Maadili ya Bunge na hatua kuchukuliwa basi itakuwa funzo kwa mawaziri wengine kuepuka kutoa tuhuma kwa wabunge pasipo kuwapo kwa ushahidi wa kutosha.

إرسال تعليق