WAPIGA KURA JIMBO LA ISIMANI WAMPONGEZA MBUNGE WAO LUKUVI KWA KUTEKELEZA VEMA AHADI ZAKE
Na Francis Godwin Blog
WANANCHI
wa jimbo la Isimani mkoani Iringa wamepongeza jitihada mbali mbali
zinazofanywa na mbunge wao Wiliam Lukuvi na kumtaka mbunge huyo
kuwawabana watendaji wasio wasio wajibika kwa wananchi.
Wananchi
hao walitoa pongezi hizo leo kwenye ukumbi wa Hima Isimani wakati
mdahalo wa wazi Kati ya mbunge Lukuvi na wananchi ,mdahalo ulioandaliwa
na asasi za kiraia Tanzania na kuratibiwa na asasi ya ISICO mkoa wa
Iringa.
Akizungunza
kwa niaba ya wenzake Maneno Kalinga alisema kuwa mbunge Lukuvi ni
mbunge pekee katika mkoa wa Iringa kwa kufanya kazi karibu na wananchi
wake ikiwa ni pamoja na kushughulikia kero za wananchi wake .
Kwani
walisema kuwa baadhi ya watendaji wa kata hiyo wamekuwa wakishinda
mjini Mara zote na kuacha ofisi jambo ambalo limekuwa ni kero kubwa kwa
wananchi .
Hivyo
walimtaka mbunge Lukuvi kuwawezesha watendaji hao wa vijiji kupata
semina ila kujua majukumu Yao badala ya kugeuka watalii katika ofisi
hizo za vijiji.
Wakati
Lucy Kaginga alieleze kusikitishwa na tabia ya walimu wa shule ya
Msingi Kising'a Isimani kuwatumikisha watoto katika shuguli za kuchota
maji kwa ajili ya kujenga nyumba ya mwalimu badala ya kusoma.
Kwani alisema kuwa tabia hiyo imekuwa ni kero kubwa kwa wanafunzi hao na wazazi wanaomba mbunge kukomesha hali hiyo.
Wakati
huo huo mbunge Lukuvi amewataka wananchi wa jimbo hilo kuweka
utaratibu wa kuchangia chakula katika shule za Msingi ili kusaidia
kuboresha Elimu kwa wanafunzi wa shule za Msingi na kupunguza Utoro kwa
wanafunzi.
Mbunge
Lukuvi ambaye ni waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu sera ya uratibu wa
bunge ametazama hayo katika mdahalo wa wazi uliofanyika katika ukumi wa
Hima kata ya Isimani mdahalo Kati ya wapiga kura wake na mbunge huyo
,mdahalo ulioendeshwa na asasi isiyo ya kiserikali ya ISICO mkoani
Iringa.
Akizungunza
kwa niaba ya mbunge huyo katibu wake Thoma Malenga alisema kuwa kero ya
wanafunzi kushinda na njaa ama kurudi nyumbani mchana kwa ajli ya
kupata chakula cha mchana linaweza kutatuliwa iwapo wananchi watakuwa na
mkakati wa kuchangia chakula kwa ajli ya watoto hao.
Kwani
alisema kuwa ili kupunguza Utoro kwa. Wanafunzi hao lazima wananchi
kuweka mkakati. Wa kuhamasishana kuanzisha mpango wa kuchangia chakula
ili watoto hao kupata chakula wakiwa shule.
Kuhusu
kero ya maji katika eneo Hilo la Isimani Alisema kuwa tayari mkakati wa
kuwaunganisha wananchi hao na mradi wa maji wa uhakika unafanyika na
wananchi wategemee kupata huduma hiyo ya maji .
Aidha
aliwataka wananchi waliowekewa alama za x katika nyumba zao kwa ajili
ya kupisha upanuzi wa barabara ya Iringa - Dodoma kujiandaa kulipwa
fidia kupitia wakala wa barabara mkoa wa Iringa ( TANROADS)
إرسال تعليق