KOCHA Andre Villas-Boas anataka aanze kazi Tottenham kwa kumsajili
kiungo mshambuliaji wa Brazil, Oscar kutoka Internacional. Mchezaji huyo
mwenye umri wa miaka 20 anapatikana kwa dau la pauni Milioni 20.
Wakati huo huo klabu ya Tottenham iko tayari kumsaidia kocha wake mpya, Andre
Villas-Boas katika soko la usajili kwa kumkatia pauni Milioni 50. Kocha
Mreno huyo anataka kuwasajili mshambuliaji wa Marseille, Loic Remy, beki
wa Ajax na Ubelgiji, Jan Vertonghen, kiungo wa Hoffenheim, Gylfi
Sigurdsson, kiungo wa CSKA Moscow na Urusi, Alan Dzagoev na kipa wa
Birmingham, Jack Butland watue White Hart Lane.
إرسال تعليق