| Miss Sinza 2012, Brigita Alfred katikati akiwa na mshindi wa pili, Judith Sangu (Kulia) na Esther Mussa (Mshindi wa tatu kushoto) pamoja na warembo wengine, Mariam Miraji na Nahma Said amabo walishika nafasi ya nne na tano. |
MREMBO
Brigita Alfred usiku wa kuamkia jana alitwaa taji la Redds Miss Sinza
baada ya kuwashinda wenzake 13 katika kinyang’anyiro kilichofanyika
kwenye ukumbi wa Mawela Social Hall (Ten Star Lounge).
Brigita
alionekana tokea mwanzo kuwa ataibuka uwa mshindi kwani aliuteka umati
wa mashabiki wa masula ya urembo katika mashindano hayo
yaliyodhaminiwa na kinywaji cha Redds, Dodoma Wine, Lady Pepeta, Flexi
P, Jackz Cosmetics, Clouds FM, sufianimafoto.blogspot.com na Screen Masters.
Kwa
ushindi huo,Brigita alipewa shs 500,000 na tiketi ya kuiwakilisha
Sinza katika mashindano ya Redds Miss Kinondoni. Mshndi wa pili katika
kinyang’anyro hicho alikuwa Judith Sangu aliyezawadiwa sh. 400,000 na
mshindi wa nafasi ya mshind wa tatu ilikwenda kwa Esther Mussa na kupewa
shs. 300,000.
Mariam
Miraji alishinda nafasi ya nne nay a tano ilikwenda kwa Nahma
Saidi. Warembo wote hao watano walipata tiketi ya kushindana katika
mashindano ya Miss Kinondoni.
Warembo
wengine waliobaki, Naima Mohamed, Lulu Ambonela, Maria John, Eva
Mushi, Vailet John, Christina Samwel, Aisha Ramadhan, Nancy Musharuzi na
Merina Mushi walipewa zawadi ya kifuta jasho cha shs 100,000 ila
mmoja katika shindano hilo lilopambwa na bendi ya African Stars wana
Twanga Pepeta
إرسال تعليق