TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
YAH: TAARIFA KUWA BAADHI YA WALIMU ‘WAMEIKACHA’ CWT SIYO YA KWELI
Gazeti la Nipashe la tarehe 9 Julai 2012 ukurasa wa pili iliandikwa taarifa yenye kichwa; Baadhi ya walimu ‘waikacha’ CWT.
Maelezo
haya siyo ya kweli maana walimu hawajajitoa (kuikacha) CWT na wale
walioshawishiwa wajitoe walishindwa maana waliahidiwa na viongozi wa
UMET kuwa mara ukiandika barua ya kujitoa makato yako ya 2%
yatasitishwa jambo ambalo haliwezekani. Kusitishwa kwa makato ni suala
la kisheria kuwa Chama kinapofikisha zaidi ya nusu ya wafanyakazi wa
sekta hiyo waliobakia wanatakiwa kukatwa 2% ya huduma kwa chama (Union
Service charge) kwa sheria Na 10 ya Vyama Huru vya wafanyakazi ya
1998 na huduma ya wakala (Agency fee) kwa sheria ya Ajira na Mahusiano
Kazini namba 6 ya 2004.
Hakuna
sheria inayoruhusu mwanachama kujitoa chama na kufuta makato na hii ni
sheria ya Bunge siyo matakwa ya CWT, maana huwezi kuwa unafaidi
matunda kwa jasho la wenzako (Free rider).
Idadi
ya wanachama wa UMET iliyotajwa kwenye gazeti la Nipashe hiyo si ya
kweli, mfano mkoa wa Mbeya kuwa na wanachama 3,641 si kweli maana
wanachama wa CWT Mbeya ni 13,833 kati ya walimu 16,934 hivyo wangekuwa
na kiasi hicho (3,641) Mbeya isingetawalika ki-CWT .
Hizo
takwimu za wanachamwa UMET wanzipataje wakati hawajasijiriwa? Je,
wanachama wao wanawajuaje? Kw mujibu wa sheria ya Ajira na Mahusaiano
Kazini ya 2004, Ili uwe mwanachama wa chama cha wafanyakazi chochote
lazima uwe umejaza fomu inayoitwa TUF 6 yaani (Trade Union Form Number
6) na baada ya hapo wanachama wanajazwa kwenye daftari la wanachama
kwa fomu namba 15. Je, hao UMET wanachama wao wamewapataje kwama siyo
propaganda na uzushi? Nadhani wanashindwa kutofautisha kati ya
wanachama na hisia za kuwa na washabiki. UMET wanadhani kila
anayemshabikia nyoka aliyeuawa anampenda nyoka kumbe wengine wanataka
kuona ukubwa na aina ya nyoka aliyeuawa.Wajaribu kuchanganua mambo kwa
mapana zaid.
Kumekuwa
na taarifa za upotoshaji kwa wanachama na walimu wenye mapenzi mema
na CWT yao juu ya vitega uchumi vya CWT. Kimsingi CWT inakitega uchumi
kimoja tu yaani jengo la ‘Mwalimu House’ lenye ghorofa kumi lililoko
Ilala Boma. Jengo hilo ni la kupangisha na mapatoi yake ni kati y
ash, 35 hadi 40 milioni kwa mwezi. Aidha, kuanzishwa kwa kampuni ya
walimu TDCL (Teachers’ D eveolpment Company Limited) wala lengo lake
si kufanya biashara bali ilianzishwa kwa lengo la kupata nafuu ya kodi
katika uwekezajiambayo ni sera ya CWT.
Mapato
na matumizi ya fedha zote za Chama yanakaguliwa kila mwaka na mkaguzi
wan je fedha toka Kampuni inayotanmbuliwa na kuwasilishwa kwa Msajili
wa vyama vya wafanyakazi. Chama kisipowasilisha ukaguzi wake wa fedha
kinafutwa. Aidha, mwanachama hazuiliwi kuuliza mapato na matumizi ya
fedha za chama kwenye ofisi za CWT hakuna siri yoyote.
Kwa
mantiki hiyo, maelezo ya UMET ni ya kupotosha walimu na inaonyesha
viongoizi wake wanatumiwa na serikali ili kuwagawa walimu wasidai
maslahi bora wakati huu ambapo CWT kimetangaza mgogoro na serikali.
Natoa
wito kwa walimu kuwa makini na makundi haya yanayotumiwa na serikali
pamoja na propaganda na vitisho mbalimbali vya serikali. Wakati
ukifika wa mgomo tuungane wote bila woga wala kulinda vyeo vyetu
serikalini kama ualimu mkuu, uratibu, ukuu wa shule, n.k. tudai maslahi
bora kwa walimu wa kizazi hiki ili tuwe tayari kutoa elimu bora kwa
watanzania. Walimu wawe macho na kila namna yoyote ya kuwagawa au
kuwachonganisha na CWT wasahau kuidai serikali maslahi bora. Kila
mwalimu anahitaji maslahi bora.
Nawatakia kazi njema na afya tele.
MSHIKAMANO DAIMA! NA NDIO MKOMBOZI WETU
Mwl. Kasuku Bilago
Katibu CWT Mkoa
Mbeya
إرسال تعليق