COASTAL UNION YATINGA FAINALI BURUNDI

COASTAL UNION YATINGA FAINALI BURUNDI


TIMU ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Coastal Union ya Tanga, leo imefanikiwa kuingia fainali ya michuano ya Rollingston, baada ya kuwafunga mabingwa watetezi, Ruvu Shooting mabao 2-1 nchini Burundi.
Mabao yote ya Coastal yalitiwa kimiani na Mohamed Miraj, wakati bao la Ruvu waliotwaa ubingwa wa michuano hiyo mwaka jana mjini Arusha, lilitiwa kimiani na Said Hussein.
Kwa matokeo hayo, Coastal itamenyana na Ecofoot ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), ambayo katika Nusu Fainali nyingine leo, waliitoa Mjini Magharibi ya Zanzibar kwa mabao 2-1 pia.
Mabao ya Ecofoot yalitiwa kimiani na Sais Kabamba na Shukuru Hamisi, wakati bao la kufutia machozi la Mjini Magharibi lilitiwa kimiani na Omar Tamim. Sasa, Mjini Magharibi itamenyana na Ruvu katika mchezo wa kusaka mshindi wa tatu na Coastal itamenyana na Ecofoot katika mechi ya kusaka bingwa mpya wa michuano hiyo keshokutwa. Chanzo:- Bin Zubery

Post a Comment

أحدث أقدم