| Kaseja akishangilia baada ya kukabidhiwa kombe la ubingwa wa Urafiki Cup |
KIPA
namba moja wa Tanzania, anaechezea Mabingwa wa Soka Tanzania Bara na
Mabingwa wapya wa Urafiki, Juma Kaseja amezidi kujidhihirisha kuwa yeye
ni tishia katika kudaka mikwaju ya penati baada ya kudaka penati mbili
kati ya 5 za Azam na kuisaidia klabu yake ya Simba kutwaa ubingwa wa
Kombe la Urafiki baada ya kushinda kwa penati 3-1 katika mechi yao ya
fainali iliyoamuliwa kwa ‘matuta’ kufuatia sare ya 2-2 katika muda wa
kawaida kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo usiku.
Kaseja
ambaye pia ni nahodha wa Simba, alidaka kiufundi penati za Waziri na
Mwaipopo huku Himid Mao akipaisha na hivyo kuipa Simba ubingwa wa
michuano hiyo ikiwa ni siku moja tu kabla ya kuanza kampeni yao ya
kuwania taji la Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kombe la
Kagame).
Mwinyi
Kazimoto, Amir Maftah na Kigi Makassy ndio waliofunga penati za Simba
huku Haruna Moshi ‘Boban’ akikosa baada ya penati yake kugonga
‘besela’, wakati aliyefunga bao la Azam akiwa ni Khamis Mcha pekee.
Katika
dakika 90 za kwanza, Simba mabao yao kupitia Felix Sunzu na Mwinyi
Kazimoto aliyefunga kwa penati huku mabao ya Azam yakiwekwa wavuni na
Mcha Khamis na John Bocco.
Kwa ushindi huo, Simba walizawadiwa kombe na fedha taslim Sh. milioni 10 wakati Azam walizawadiwa Sh. milioni 5.
Vikosi:
Simba:
Juma Kaseja, Shomari Kapombe/Haruna Shamte (dk.45), Amir Maftah,
Mungusa, Juma Nyoso, Mussa Mudde/Haruna Moshi ‘Boban, Amri Kiemba,
Mwinyi Kazimoto, Salim Kinje/Uhuru Selemani(dk.61), Felix Sunzu/Kigi
Makassy (dk.74) na Abdallah Juma/Danny Mrwanda (dk.45).
Azam:
Deogratias Munishi, Ibrahim Shikanda, Waziri Juma, Said Moradi, Joseph
Owino/Agrey Morris (dk.45), Ibrahim Mwaipopo, Kipre Bolou/Jabir Aziz
(dk.66), Ramadhani Chombo ‘Redondo’, Kipre Tchetche/John Bocco (dk.45),
George Odhiambo na Khamis Mcha.
إرسال تعليق