|
SIMBA
SC imetwaa ubingwa wa Kombe la Urafiki, baada ya kuifunga Azam FC kwa
penalti 3-1 usiku huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, kufuatia
sare ya 2-2 ndani ya dakika 90.
Penalti
za Simba zilikwamishwa nyavuni na Mwinyi Kazomoto, Amir Maftah na Kiggi
Makassy, wakati Haruna Moshi Boban alipaisha na kwa upande wa Azam FC,
aliyefunga ni Hamisi Mcha ‘Vialli’ pekee, wakati Samir Hajji Nuhu
ilidakwa na Juma Kaseja, Ibrahim Mwaipopo ilipanguliwa na Himid Mao
‘iliota mbawa’.
Kabla
ya matuta, mshambuliaji wa kimataifa wa Zambia, Felix Sunzu alitangulia
kuifungia Simba dakika ya 29 kabla ya Hamisi Mcha ‘Vialli’ kusawazisha
dakika ya 45 na ushei.
Kipindi cha pili mchezo ulichangamka zaidi na dakika ya 81, John Bocco
‘Adebayor’ aliyetokea benchi aliifungia Azam bao la pili, kabla ya
Kazimoto kuisawazishia Simba kwa penalti dakika ya 87, baada ya Danny
Mrwanda kuangushwa kwenye eneo la hatari.
Kwa ushindi huo, Simba SC wamezawadiwa Sh. Milioni 10 na Azam FC Milioni 5.
|
إرسال تعليق