KLABU ya Liverpool imekubali dili la pauni Milioni 12 kumnasa
Fabio Borini, mwenye umri wa miaka 21, awe mchezaji wa kwanza kusajiliwa
na kocha wao mpya, Brendan Rodgers, na Mtaliano huyo anatarajiwa
kukamilisha usajili wake mwishoni mwa wiki.
KUSAJILIWA kwa Fabio Borini kutahitimisha zama za Craig Bellamy katika
Uwanja wa Anfield, na QPR na Cardiff zote zinaiwania saini ya
mshambuliaji huyo wa Liverpool.
إرسال تعليق