Staa
wa hip hop Bongo, Godzilla ameongea kuwa hatua ya kutoa wimbo ukiwa
kwenye staili ya kuimba imekuja kufuatia maombi kibao aliyoyapata kutoka
kwa mashabiki wake.
Akizungumza hii leo Godzilla anayesumbua
kitaa na ngoma kali inayobeba jina la ‘La Kuchumpa’ amesema kuwa
ameshangazwa na hatua ya wadau wa muziki wa kizazi kipya kuhoji juu ya
uamuzi wake wa kutumia staili ya kuimba kwenye wimbo wake mpya uliopewa
jina la ‘nataka’.
“Unajua mimi ni mwanamuziki na katika hilo ni lazima ujue kuwa nina
mashabiki ambao kwa lolote wako nyuma yangu , hivyo basi walinifuata na
kuniambia kuwa wanataka nijaribu kutoa wimbo kwenye staili ya kuimba soo
kwakuwa ninatambua umuhimu wao nikaamua kutoa nyimbo mbili moja ikiwa
kwenye mtindo huo na nyingine ikiwa kwenye hip hop kama kawaida” alisema
Zilla na kuongeza kuwa nimeamu a kufanya hivyo ili kuwarizisha
mashabiki wangu wote
إرسال تعليق