Nyota wa muziki wa kizazi kipya Bongo, ALLY Timbulo ‘Timbulo’ amepatwa na
tukio la aina yake baada ya wajanja wa Bush kumliza kamera kubwa aina
ya sonny wakati wa paty maalumu aliyoifanya mwishoni mwa wiki
iliyopita kijijini kwao Riuwa, Wilayani Mbalali jijini Mbeya.
Akizunguma leo mapema Timbulo amesema kuwa aligundua kupotea ghafla
kwa kamera yake hiyo mara baada ya kumalizika kwa paty hiyo iliyokuwa
imechangamka kupita kiasi huku vijana wengi aliokuwa wamefurika wakiwa
hoi kwa mitungi.
“Nilipomaliza kuimba nikawa nimechili sehemu napumzika, lakini
baada ya party kuisha nianza kukusanya vitu vyangu na baadae nikagundua
kuwa kamera yangu haipo, kwa kweli nilichanganyikiwa kwa kuwa bado ni
mpya kabisa na niliinunua kiasi cha dola 800 za Marekani” alisema
Timbulo
Akiendelea zaidi timbulo amesema kuwa juhudi za kumsaka mtu
aliyesepa na kamera hiyo ya kisa bado zinaendelea kwa kuwa sehemu kubwa
ya watu waliofika siku hiyo wanafahamiana hivyo anaamini ndani ya siku
chache zijazo atakuwa ameipata.
katika shoo hiyo Timbulo amerifu kuwa jukwaa alilokuwa
analitumia kuwaburudisha mashabiki wake lilishindwa kuhimili vishondo
na kuvunjika kufuatia watu kushindwa kuvumilia na kupanda juu
alipokuwa yeye na hatimaye jukwaa hilo likasalimu amri.
“Hakika ilikuwa siku mbaya kwani kuna mambo mengi
yalijitokeza ikiwamo shughuli yangu kucheleweshwa baada ya mchana na
kuwa ucku kutokana na mtendaji wa kata kuzuia mpaka diwani alipoingilia
kati na kuniruhusu” alimaliza
Chanzo:- http://www.teentz.com
إرسال تعليق