| Victa costa(Kushoto) akiwa na Juma Kaseja(Kulia) |
BEKI wa kati wa Simba, Victor Costa amesema yupo tayari kuvunja mkataba
na mabigwa hao kama watalimpa haki zake zote anazostahili.
Costa aliyasema hayo baada ya juzi Makamu Mwenyekiti wa Simba, Godfrey Nyange 'Kaburu' kutangaza kukatisha mkataba wa beki huyo baada ya kupata ushauri kutoka kwa kocha wao Cirkovic Milovan.
Costa aliiambia alisema kuwa kwa upande wake mpaka jana alikuwa hajapata taarifa yoyote ya kuvunjwa kwa mkataba wake na wala hajakutana na viongozi wa Simba kuzungumzia suala hilo.
''Sijapata taarifa yoyote mpaka sasa labda 'leo jioni' jana ndio nitakutana na viongozi, nitakubali kuvunja mkataba kama tutakubaliana kunilipa kiasi cha fehda tulichokubalina ambacho siwezi kukiweka wazi kwenye magazeti,'' alisema Costa.
Costa alijiunga na Simba mwaka 2011 na kusaini mkataba wa miaka mitatu akitokea Ferrovoviario de Nampula ya Msumbiji.
Katika hatua nyingine Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limetoa Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) kwa Watanzania saba kucheza soka ya kulipwa katika nchi za Kenya na Msumbiji.
Afisa Habari wa TFF, Bonifasi Wambura alisema TFF, imetoa hati hizo kwa wachezaji hao baada ya kuombewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu la Kenya (FKF) na Shirikisho la Mpira wa Miguu la Msumbiji (FMF) ili waweze kucheza katika klabu za nchi hizo.
Wambura aliwataja wachezaji ambao wameombewa ITC ni ni David Naftali (huru), Meshack Abel (huru), Mohamed Banka (huru) na Thomas Mourice (Mtibwa Sugar) Bandari ya Mombasa.
Huku Klabu ya CD Madchegde ya Msumbiji ikiwachukua wachezaji wa tatu ambao ni Hassan Hassan Mustapha kutoka Mgambo Shooting ya Tanga, Abdallah Ally Abdallah na Thobias David Silas kutoka klabu ya daraja la kwanza ya Transit Camp ya Dar es Salaam.
Pia, Wambura alizikumbusha klabu kuzingatia muda wa usajili kwa wachezaji wa nje ya Tanzania kuwa ni Julai 30 na mpaka sasa mchezaji mmoja George Odhiambo wa Azam ambaye ni raia wa Kenya ndio kaombewa ITC na tayari hati hiyo imetolewa na Chama cha Mpira wa Miguu cha Denmark (DBU) ambapo Odhiambo alikuwa akicheza nchini humo kabla ya kutua Azam kwa ajili ya msimu wa 2012/2013.

إرسال تعليق