THEA AJIFUNGUA MTOTO SIYO RIZIKI


MSANII mwenye heshima kunako tasnia ya filamu za Bongo, Ndumbangwe Misayo ‘Thea’ (pichani) amejifungua lakini mtoto wake akiwa amefariki dunia.

Chanzo chetu makini kilichoomba hifadhi ya jina lake kilieleza kuwa, Thea alijifungua mtoto wa kike kwa njia ya kawaida usiku wa kuamkia Jumanne iliyopita katika Hospitali ya Marie Stopes lakini akawa siyo riziki.

Aidha, chanzo hicho kiliongeza kuwa mwili wa kichanga hicho ulizikwa katika Makaburi ya Mwananyamala jijini Dar juzi Jumanne asubuhi.

Jitihada za kuwapata Thea au mumewe Mike Sangu ili kuzungumzia ishu hiyo hazikuzaa matunda hadi tunakwenda mtamboni

Post a Comment

أحدث أقدم