SHEREHE ZA UFUNGUZI OLYMPIC LONDON LEO HII
Familia
ya kifalme imeukaribisha mwenge wa Olimpiki katika Kasri la Buckingham
katika siku ambapo umati mkubwa wa watu ulikusanyika mjini London
kushuhudia mkondo wa mwisho wa safari ya mwenge huo mjini London.
Mwenge huo kadhalika uliwasilishwa Downing Street, makao makuu ya serikali ya Uingereza.
Baada
ya tetesi kuzuka kuhusiana na maandalizi ya michezo hiyo, waziri mkuu
wa Uingereza David Cameron amesema michezo ya mwaka huu itathibitisha
kuwa Uingereza ina uwezo wa kufanya maandalizi kabambe.
Leo Ijumaa ndiyo siku ya ufunguzi rasmi wa mashindano yatakayopeperushwa moja kwa moja kote duniani.
Bwana
Cameron ametetea maandalizi ya mashindano hayo baada ya mgombea wa kiti
cha urais nchini Marekani Mitt Romney kusema kwenye mahojiano katika
runinga ya NBC kwamba kuna matatizo katika usalama na tishio la mgomo wa
maafisa katika maeneo ya mipakani.
Lakini baadaye bwana Romney
alitabiri kuwa mashindano ya Olimpiki mjini London yatakuwa yenye
mafanikio baada ya kukutana na waziri mkuu huko Downing Street.
Hapa Bw. Cameron aliukaribisha mwenge huo wakati uliposimama kwa muda ukiwa njia kuelekea Kasri la Buckingham.
Mwanamfalme
William, mkewe na mwanamfalme Harry walikuwepo kuwakaribisha waliokuwa
wakiiperusha mwenge huo kabla ya kupelekwa Hyde Park.
Meya wa
mji wa London Boris Jonnson akizungumza mbele ya umati mkubwa wa watu
60,000 waliojitokeza kushuhudia sherehe hiyo aliwatakiwa kila la heri na
kusema ''mashindano ya London yatakuwa ni ya kukata na shoka.''
Lakini
pia alizungumzi mzozo uliokuwepo awali aliposema mbele ya umati huo:
"kuna mtu anayeitwa Mitt Romney ambaye anataka kujua ikiwa tuko tayari.
Tuko tayari? Ndiyo tuko Tayari!"
إرسال تعليق