URA YATINGA ROBO FAINALI KAGAME,
![]() |
| Wachezaji wa URA wakishangilia bao la tatu |
URA ya Uganda, imekuwa timu ya kwanza kufuzu Robo Fainali ya
Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame kutoka Kundi A, baada ya
kuichapa mabao 3 -1, AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam jioni hii.
Mabao ya URA yaliwekwa wavuni na Sula Bagala (mawili) na
Robert Ssentongo, wakati la kufutia machozi la Vita, inayofundishwa na kocha wa
zamani wa Yanga, Raul Jean Pierre Shungu lilifungwa na Mutombo Kazadi.
URA sasa imefikisha pointi sita baada ya kucheza mechi mbili na kushinda
zote na itamaliza na Ports ya Sudan kutafuta kujihakikishia
uongozi wa kundi hilo tu.

إرسال تعليق