Alichokisema Dkt. Lwaitama na Prof. Shiviji ni hiki hapa
Sikuwahi kusikia mahali
popote ambapo Prof Sheriff alitamka kuwa eti “anataka” Muungano uvunjwe,
yeye kama yeye. Sasa huyu mwandishi Datus Boniface halipata wapi
ujasiri wakumlisha mwanataaluma ya historia huyu wa Kitanzania, hata
kama ni Mzanzibari pia? Uandishi wa habari wa aina hii ya Datus Boniface ni wa kusikitisha sana.
Tamko la DKt. Lwaitama kuhusu habari ya “Shivji, Lwaitama wataka Muungano uvunjwe”
11/08/2012
JUU YA MUUNGANO: TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
11/08/2012
JUU YA MUUNGANO: TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Nimesikitishwa na aina ya uandishi wa habari uliojiweka wazi katika
taarifa iliyonukuliwa kuandikwa na mwandishi wa gazeti moja la kila
siku (Tanzania Daima la tarehe7 Agosti 2012), Datus Boniface. Huyu
mwandishi, pamoja na wahariri wake walioruhusu habari hiyo kuchapwa
walithubutu kusema uongo kuwa eti “Dk Lwaitama, Prof. Sheriff na Prof
Shivji waliushambulia Muungano..” Tena, mwandishi huyu na wahariri
walioruhusu habari hiyo ichapishwe wakaenda mbali zaidi na kutumia
kichwa cha habari kilichosema eti ‘Shivji, Lwaitama wataka Muungano
uvunjwe’.
Nafahamu Prof Shivji tayari ameisha toa tamko juu ya:- Zaidi bofya hapa zanzibaryetu.wordpress.com
إرسال تعليق