MBUYU TWITE KUMSHITAKI NA SIMBA
Hanspop |
KLABU ya Simba imesema itamfikisha mahakamani mchezaji Mbuyu
Twite wa klabu ya APR kwa kosa la kuwatapeli na kukubali kusajiliwa na Yanga.
Mwenyekiti wa kamati ya Usajili ya Simba, Zakaria Hanspope amekaririwa
na liwazozito.blogspot.com akisema,
Twite alishapokea fedha za Simba na kukubali kuingia nayo mkataba, hivyo hawezi
kwenda kinyume.
Hanspope alisema kilichofanywa na Yanga kumshawishi mchezaji
huyo arejeshe fedha za Simba na kupokea fedha zao ni cha kihuni na hawawezi
kukivumilia.
Alisema kama ni kurejesha fedha zao, anayepaswa kufanya
hivyo ni Twite mwenyewe na si klabu ya Yanga.
Hanspope alisema wao waliingia mkataba na Twite kupitia klabu
yake ya APR na Shirikisho la Soka la Rwanda, hivyo walipaswa kuomba hati ya
uhamisho kutoka Rwanda na si Congo.
"Haya mambo lazima ufike wakati yafikie mwisho.
Haiwezekani klabu imesikia kwamba mchezaji amesajiliwa na klabu fulani na
yenyewe inamfuata kuzungumza naye,"alisema.
Hanspope alisema bado wanaamini kwamba Twite ni mchezaji wao
na kama itatokea vinginevyo, watapambana hadi haki yao ipatikane.
Yanga imemsajili Twite, wakati tayari akiwa amekwishaini
Simba SC, baada ya kumrudisha kwenye uraia wake wa asili, Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo (DRC), badala ya Rwanda aliopewa wakati akicheza nchini
humo na kumbadili jina pia.
Kwa kumbadili uraia, Yanga walipata na Hati ya Uhamisho wa
Kimataifa (ITC) ya mchezaji huyo, kutoka Shirikisho la Soka (DRC), na kuwaacha Simba
wakihangaika bila mafanikio kupata ITC ya mchezaji huyo kutoka FERWAFA,
Shirikisho la Soka la Rwanda.
Yanga inamsajili Twite kama mchezaji kutoka St Eloi Lupopo,
klabu ambayo aliichezea kabla ya kutua APR mwaka 2006 kwa pamoja na ndugu yake,
Kabange. Lakini mchezo uliochezwa hapa ni kwamba Twite alikuwa anacheza kwa
mkopo APR.
Habari zaidi zinasema, Yanga inamsajili pia na pacha wake
Mbuyu (pacha wa kuzaliwa kabisa), Kabange, kwa sababu wachezaji hao kawaida yao
kucheza timu moja daima.
Huko nyuma, Yanga iliwahi kuifanyia tena Simba ‘umafia’ kama
huu katika usajili wa wachezaji, Charles Boniface Mkwasa na Yussuf Ismail Bana,
miaka ya 1980.
Simba ilimsaiji beki wa Pamba kama Yussuf Bana, lakini Yanga
wakaingilia kati na kumsajili kwa jina la Yussuf Ismail Bana, Mwenyekiti wa
Chama cha Soka Tanzania (FAT, sasa Shirikisho, TFF), wakati huo Said Hamad El
Maamry akamuidhinisha beki huyo kucheza Yanga
إرسال تعليق