
Oribe Peralta aliipatia Mexico bao la kwanza ikiwa ni sekunde 29 baada ya kipenga cha kuanza mchuano kupulizwa.
Peralta litumia fursa iliyotokana na kosa la
beki wa Brazil kuchezea katika nusu ya uwanja kwa upande wa Brail na
kuikandika Brazil bao la haraka lililozipeleka pande hizi hadi mapumziko
kwa hesabu ya 1-0 kwa Mexico.

Bao la Peralta
Hili ni bao la kwanza kufungwa haraka zaidi katika kipindi cha miaka 36 ya mashindano ya soka ya Olimpiki.
Mshambuliaji huyo huyo alirudi kutikisa nyavu za Brazil mnamo dakika ya 75 kwa mpira wa kichwa.
Brazil ilipata bao lake la kufutia machozi
kupitia mshambuliaji Givaldino Hulk zikisalia dakika kama tatu hivi
kufikia mwisho wa mechi lakini Mexico ikashikilia mabao yake mawili hadi
kipenga cha mwisho.

Mexico yafurahia ushindi
Kabla ya mechi hii, watangazaji wa idhaa ya
kiswahili walitabiri ushindi wa Brazil, lakini Mexico ilikuwa na mipango
tofauti na fikra za wengi.
Hivyo basi historia inabaki pale pale kwa Brazil
kuondoka mashindano haya ya Olimpiki bila medali ya dhahabu ingawa
itaondoka na fedha.
Jumla ya watu 86,162 wameshuhudia pambano hili
ikiwa ni idadi kubwa kuwahi kuhudhuria mechi yoyote kwenye mashindano
haya ya Olimpiki ya London 2012. Jumla ya watu milioni 2,186,930
wamehudhuria mashindano ya mpira ya wanawake na wanaume kwenye Olimpiki
hizi.
إرسال تعليق