APONEA CHUPU CHUPU KUPIGWA CHINI MTANASHATI ENTERTAINMENT - SUMA MNAZARETI

APONEA CHUPU CHUPU KUPIGWA CHINI MTANASHATI ENTERTAINMENT - SUMA MNAZARETI
Rapper wa kampuni ya Mtanashati Entertainment, Suma Mnazareti nusura apigwe chini na uongozi kwa kukiuka miongoni mwa masharti yaliyowekwa kwenye mkataba wake.

Sharti alilolivunja ni kuchukua uamuzi wa kusambaza video yake mwenyewe kazi ambayo ilitakiwa kufanywa na meneja wa kampuni hiyo.

Akiongea na Power Jams ya East Africa Radio jana, Mkurugenzi wa kampuni hiyo Ustaadh Juma alisema, “Kiufupi msimamo wa Mtanashati ni kwamba sisi tuna menejimenti maalum. 

Msanii anapotoa nyimbo, meneja anaanza kuipeleka kila media ianze kufanyiwa kazi kwa nidhamu maalum na video pia itasimamiwa kwa nidhamu maalum, na meneja wetu ndiye atasambaza video kwa nidhamu maalum.”

Amesema Suma alikuwa hajajua utaratibu huo na tayari baada ya kuonywa ameomba radhi na amesamehewa.

“Lakini napenda kusema kwamba, ikiwa msanii yeyote anajua anatoka Mtanashati harusiwi kuleta yeye mwenyewe kazi kwa mkono. 

Msanii atakayekuja basi media naomba zifahamu kwamba msanii ameenda kinyume na utaratibu wa Mtanashati na ni kinyume cha nidhamu,” alisisitiza Ustaadh Juma

Post a Comment

أحدث أقدم