AZAM FC WAMTMUA BLACKBERRY
![]() |
Odhiambo 'Blackberry' |
AZAM
FC imevunja mkataba na kiungo George Odhiambo ‘Blackberry’, baada ya
mchezaji huyo wa Kenya kukiuka mkataba wake, kitendo ambacho
kimechukuliwa kama ni utovu wa nidhamu, imeelezwa.
“Blackberry
hajaonekana mazoezini siku sita na kwa sababu hiyo, klabu imevunja naye
mkataba. Huyu mchezaji kwa kweli ametuangusha sana,”alisema kiongozi
mmoja wa Azam.
Pamoja
na kusajiliwa kwa matumaini makubwa, kiungo huyo bora wa zamani wa Ligi
ya Kenya, alishindwa mapema tu kudhihirisha uwezo wake katika soka ya
Tanzania, kuanzia kwenye Kombe la Urafiki na baadaye Klabu Bingwa Afrika
Mashariki na Kati, Kombe la Kagame.
Kwa
kuondolewa Blackberry, Azam sasa inabaki na wachezaji wanne wa kigeni,
ambao ni mabeki Ibrahim Shikanda kutoka Kenya, Joseph Owino kutoka
Uganda na viungo Kipre Michael Balou na Kipre Herman Tchetche kutoka
Ivory Coast.
Kuna uwezekano Azam ikasajili mshambuliaji mwingine kutoka Ivory Coast, kuziba nafasi ya Odhiambo.
إرسال تعليق