MAGAZETI YA LEO ULAYA NA TETESI ZA UAMISHO(BACA, EVARTON, CHELSEA, LIVERPOOL, ARSENAL NDANI)

KINDA LA UFARANSA LAZIRUKA ARSENAL, AC MILAN, SPURS KUELEKEA EVERTON

M'Baye Niang Kocha wa Everton, David Moyes anataka kumsajili kinda wa umri wa miaka 17, Mfaransa M'Baye Niang kwa dau la pauni Milioni 2 kutoka Caen.

Chelsea imeiambia Barcelona kwamba beki David Luiz hauzwi kwa bei yoyote.
Mchezaji wa Middlesbrough, Marvin Emnes na Tom Ince wa Blackpool wanatakiwa sana na Swansea City.

OBI MIKEL AIPA UBINGWA CHELSEA LIGI KUU

Kiungo wa Chelsea, John Obi Mikel anaamini mbio za ubingwa wa Ligi Kuu zitakuwa ngumu msimu huu lakini amesistizaThe Blues wanaweza kuibuka mabingwa.
Theo Walcott yupo kwenye mazungumzo na Arsenal juu ya mkataba mpya wa miaka mitano kuendeleea kuishi Emirates.
Habari kamili: Daily Mirror
Mshambuliaji wa Liverpool, Luis Suarez amesema kwamba yupo katika timu nzuri, ingawa ana hasira uwanjani.
Habari kamili: Guardian 

Post a Comment

Previous Post Next Post