MAN UNITED WAIPIGA BAO NJE YA UWANJA MANCHESTER CITY
Kocha wa Manchester United, Sir Alex Ferguson amewapiku jirani
zake, Man City katika kuwania saini ya mshambuliaji wa Chile, Angelo
Henriquez, mwenye umri wa miaka 18.
Arsenal inajipanga kumruhusu Robin van Persie, mwenye umri wa miaka 29,
kujiunga na Manchester United kwa dau la pauni Milioni 22.
Habari kamili: the Sun
Lakini taarida nyingine zinasema kwamba Arsenal wanataka angalau
pauni Milioni 25 kutoka Manchester United kwa ajili ya Van Persie.
Habari kamili: Evening Standard
Manchester City inafikiria kuongeza vipaji zaidi vya Kiingereza
kwenye kikosi chake, baada ya kumsajili Jack Rodwell na Scott Sinclair,
Jack Butland na Nathan Redmond wakiwa wanatajwa kufuatiliwa na mabingwa
hao wa Ligi Kuu ya England.
Habari kamili: Daily Mail
Everton inataka kutumia sehemu ya fedha ilizopata kutokana na mauzo ya
Jack Rodwell, mwenye umri wa miaka 21, kwenda Manchester City kwa
kumsajili Kevin Mirallas, mwenye umri wa miaka 24, kutoka Olympiacos kwa
dau la pauni Milioni 6.
Habari kamili: The Times
Liverpool imemtuma Mkurugenzi wake Mtendaji, Ian Ayre kwenda
Hispania kushughulikia usajili wa winga wa Barcelona, Cristian Tello,
mwenye umri wa miaka 21, na kiungo wa Real Madrid, Nuri Sahin, mwenye
umri wa miaka 23.
Habari kamili: Metro
إرسال تعليق