MBIVAYANGA, MRWANDA WATEMWA YASAJILI BEKI MKENYA NA STRIKER LA IVORY COAST - SIMBA
Paschal Ochieng |
SIMBA SC imevunja
mkataba na kiungo Kanu Mbivayanga kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC)
na mshambuliaji mzalendo Danny Mrwanda na kusajili wachezaji wawili wengine wa
kigeni, beki Paschal Ochieng na mshambuliaji Daniel Akuffo kutoka Ivory Coast.
Mshambuliaji kutoka Hearts Of Oak ya Ghana tayari yupo Dar es Salaam tangu saa 3:00 asubuhi na jioni ya leo
atakwenda kuungana na kikosi cha Simba kilichopo kambini Arusha, wakati Ochieng
kutoka AFC Leopard ya Kenya tayari mtu amekwenda kumpokea mpakani, Namanga.
Kwa maana hiyo, Simba
sasa inakuwa na wachezaji wa kigeni watano, baada ya Waganda Emmanuel Okwi, Mussa
Mudde na Mzambia Felix Sunzu.
Habari za ndani kutoka
Simba SC, zimesema kwamba marekebisho hayo ya usajili yanatokana na
ushauri wa Kocha Mkuu wa klabu hiyo, Profesa Milovan Cirkovick, raia wa Serbia.
Cirkovck ameamua
kumuondoa kwenye kikosi chake Mrwanda, kwa sababu amempata Mrisho Ngassa na
Kanu ametemwa kwa sababu timu ina viungo wengi, hivyo ameona bora kuongeza beki
mmoja na mshambuliaji.
Wakati huo huo, kiungo
Kiggi Makassy aliyesajiliwa kutoka Yanga, sasa anahamishiwa kwenye nafasi ya
beki ya kushoto akagombee namba na Amir Maftah na Paul Ngalema.
Beki wa kulia, Haruna Shamte
ana asilimia sawa za kubaki au kutemwa kwenye kikosi cha Simba, kwani Cirkovick
anaona bora kuwatumia wachezaji wa Simba B, ambao wanafanya vizuri na wapo hadi
timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20, Ngorongoro Heroes.
Katika beki ya kati,
baada ya kumpata Ochieng, Milovan anaamini akiungana na Juma
Nyosso, Shomary Kapombe
na Obadia Mungusa atakuwa ana ukuta umara.
Lakini Milovan Zaidi bofya hapa
إرسال تعليق