RAIS Mstaafu Benjamin Mkapa, ameitaka Serikali kushirikiana na wadau wa
sekta binafsi katika mchakato wa kusaini Mkataba wa Ushirikiano na
Makubaliano ya Uchumi (Epa) kati ya nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki
(EAC) na Umoja wa Ulaya (EU). Habari na:- http://www.mwananchi.co.tz
Rais Mkapa aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati wa sheherehe ya siku ya Sekta Binafsi iliyoandaliwa na Shirikisho la Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), huku akitaka kabla ya kusaini makubaliano hayo lazima kuweka maslahi ya taifa mbele.
“Mnatakiwa kuwa makini kuhakikisha maslahi ya taifa letu yanakuwapo, hilo ndilo linalotakiwa kuwekwa mbele kwani bila kufanya hivyo tutajiweka matatani,” alisema Mkapa na kuongeza:
“Kutokufanya hivyo mtawapa nafasi hawa EU kufanya wanalolitaka katika nchi zetu, hivyo mkijipanga kama EAC na kuwa na sauti moja hakika mtawatendea haki wananchi.”
Rais Mkapa alisema madhara ya kusaini mkataba huo ni kuwapa nafasi kuingiza bidhaa zao nchini bila kuwapo kodi yeyote, kitendo ambacho kitasababisha kukosa mapato kwa taifa.
“Kwanza mtanakiwa kutambaua hawa EU wanataka nini kutoka kwetu na sisi tunataka nini, mkijua hilo mtahakikisha mnatetea wananchi wenu,” alisema Rais Mkapa na kuongeza:
“Kwanza mnatakiwa kuhakikisha wawekezaji wa ndani wanakuwa tofauti na wageni, ili kuleta tofauti na maendeleo ya jamii na taifa kwa ujumala, kwani kuna baadhi ya wawekezaji wa kigeni wanafanya kazi ambazo zinaweza kufanywa na wetu.”
Kwa upande wake, Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko, Dk Abdallah Kigoda alisema wamesikiliza maoni ya wadau na watahakikisha wanayafanyia kazi kwa mstakabali wa maendeleo ya taifa.
Dk Kigoda alisema hakuna nchi yeyote duniani iliyopiga hatua ya maendeleo bila ya kushirikisha sekta binafsi, hivyo wanatambua mchango wao na wataitumia kikamilifu.
“Tutaangalia matatizo yanayowakumba pale wanaposafirisha bidhaa zao kwenda nchi za nje hususan za EAC, ili kuhakikisha tunaondoa na kudumisha ushirikiano wetu,” alisema Dk Kigoda

Post a Comment