NEWS; NGASSA ATUA SIMBA KWA MILIONI 25

NEWS; NGASSA ATUA SIMBA KWA MILIONI 25


Ngassa sasa wa Simba
MRISHO Khalfan Ngassa ameuzwa Simba kwa dau la Sh. Milioni 25 mchana wa leo, Azam imethibitisha.
Habari za ndani kutoka Azam, zimesema kwamba Simba wamelipa fedha hizo na wamesainiwa fomu za uhamisho na sasa Mrisho anafuata nyayo za baba yake Khalfan Ngassa, ambaye aliichezea Simba SC 1991/1992.
Azam ilifikia uamuzi wa kumuuza Ngassa, baada ya mchezaji huyo iliyesajiliwa kutoka Yanga miaka miwili iliyopita, kubusu jezi ya Yanga baada ya kufunga bao la pili katika Nusu Fainali ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame, dhidi ya AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC),uamuzi huo, ni wa mzee Said Salim Bakhresa mwenyewe, ambaye alikerwa na kitendo hicho akawaagiza wanawe, Wakurugenzi wa bodi ya timu wamuuze mchezaji huyo popote, haraka iwezekanavyo.

Post a Comment

Previous Post Next Post