MKONGWE Thierry Henry, amesisitiza kuwa Arsenal inaweza kuziba vizuri
pengo la mshambuliaji wake, Robin van Persie iwapo ataondoka Emirates.
Bosi,
Arsene Wenger anatarajia kufanya mazungumzo na Van Persie wiki hii,
lakini nyota huyo wa Uholanzi bado dhamira yake ya kuondoka iko
palepale.
Klabu za Manchester City, Manchester United na Juventus
zote zinahitaji kuinasa saini ya Persie, mfungaji bora wa Ligi ya
Barclays msimu uliopita.
Henry, aliyecheza Arsenal kwa mafanikio
makubwa katika kipindi cha miaka nane na kuondoka mwaka 2007 kabla ya
kurudi kwa mkopo Januari mwaka huu, amesema kuna kila sababu ya Arsenal
kubaki imara hata kama Robin ataamua kuondoka.
"Tunatumaini
atabaki, ndivyo ilivyo," alisema Henry, raia wa Ufaransa."Sifahamu nini
hasa kinachoendelea, lakini nikiwa kama shabiki wa Arsenal, ningependa
kumwona anabaki Emirates."
"Yeye bado kwa sasa ni mchezaji wa
Arsenal, na bosi ndiye anayesimamia suala lake. Napenda kuiona Arsenal
ikifanya vizuri. Robin atafanya atakachoweza na sisi tuko tayari
kusubiri kuona.
"Nilipoondoka kila mmoja alilia, lakini mwaka
mmoja baadaye Arsenal ilikuwa mbele kwa tofauti ya pointi nane kwenye
msimamo. "Watu wanakuja na kuondoka, maisha ndivyo yalivyo."
Henry
amesema angependa kumwaona kiungo wa kimataifa wa Arsenal na England,
Jack Wilshere anayesumbuliwa na matatizo ya kifundo cha mguu na goti
anapata nafuu mapema.
Wilshere anatarajia kurejea uwanjani Oktoba baada ya kutumia msimu mzima uliomalizika akipatiwa matibabu.
Post a Comment